SoC02 Jiwe La Msingi 2: Ukombozi wa Fikra, Elimu na Uchumi

SoC02 Jiwe La Msingi 2: Ukombozi wa Fikra, Elimu na Uchumi

Stories of Change - 2022 Competition

onea 22

Member
Joined
Jul 31, 2020
Posts
34
Reaction score
20
Kwa wingi wa changamoto hizo na kuendelea kukua kwa kasi kwa hizo changamoto bila shaka lazima kutakuwa na sehemu moja ambayo ndio mzizi mkuu wa matatizo mengine yote.

Kuna usemi usemao, “Kama una changamoto nyingi zinakuandama kwa wakati mmoja, tuliza akili yako vizuri, kwani suluhisho la changamoto zako zote linaweza kupatikana kwa kutatua changamoto moja tu ambayo ndio chanzo cha changamoto nyingine.”

Wataalamu wa programu za kompyuta katika teknohama (computer programming) wanaweza kuelewa kwa urahisi zaidi mfano huu, kwani hali hiyo huwa inawatokea mara nyingi wakati wa kuandika (programe codes) za program fulani.

Kosa la kutoweka mkato au nukta sehemu moja tu, inaweza kuzua makosa mengine hata elfu moja au zaidi. Ili kutatua hayo makosa utahitajika kutuliza akili yako, kuigundua na kuirekebisha hiyo nukta au mkato mmoja tu, kisha mengine yote yatakuwa yamesawazika.

Ngoja nitoe mfano mwingine rahisi; mtu mwenye malaria huwa anahisi homa, mwili kuwa na joto, kuumwa kichwa, kutapika n.k. Kumtibu mtu wa aina hii huwa hatumpatii Panadol ili atibu kichwa wala hatumuwashii feni ili kupoza joto la mwili wake bali njia sahihi ni kutibu hiyo malaria kwa dawa zinazotatikana.

Ukitizama kwa makini changamoto zilizoainishwa ili zitatuliwe kwenye MDG’s utagundua kwamba kwa Tanzania na nchi nyingine za dunia ya tatu umasikini/ufukara ndio chanzo kikuu cha changamoto nyingine zote.

Kutokana na umasikini upatikanaji wa elimu umekuwa duni hasa kwa watu wa kipato cha chini, kutokana na umasikini huduma za afya kwa kinamama na watoto zimekosa ubora na kupelekea vifo vya kinamama na watoto, kutokana na umasikini kumekuwa na ongezeko la vitendo vya uhalifu watu wakijaribu kutafuta nafuu ya maisha kwa wizi na utapeli.

Kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania changamoto ya ufukara na njaa iliyopindukia inaendelea kuongezeka.

Hii inatokana na upungufu mkubwa wa ajira unaozikabili nchi hizo sambamba na uzalishaji mdogo wa chakula. Changamoto hizi zimepelekea vijana wengi kukimbilia nchi zilizoendelea. Wapo waliowahi kufikia kusema kwamba; “bora kuzaliwa mbwa Ulaya kuliko kuzaliwa binadamu Afrika.”

Watanzania wengi hasa vijana wamekuwa watumwa wa mfumo uliopo kiasi kwamba wamefumbwa macho wasiweze kuona au kukumbuka mahitaji yao ya msingi ni yapi kama wanadamu.

Ni wimbo ambao tumekuwa tukiimba tangu tupo darasa la tatu kwamba mahitaji ya msingi ya mwanadamu ni mavazi, malazi na chakula. Ni vitu vidogo sana tukiviangalia kwa haraka haraka lakini vitu hivyo ndivyo vinavyopelekea ulimwengu mzima watu unahangaika huku na kule ili tu kuwa na uhakika wa hayo mahitaji.

Mwanadamu yeyote akishaweza kuvipata vitatu hivyo basi walau ataishi maisha ya amani duniani. Vingine ni ziada tu ambazo zinafanya maisha yawe ya furaha hapa duniani. Vitu kama pombe, internet na mengineyo vyote hivyo ni ziada tu. Kukosekana kwa mahitaji tajwa hapo juu tutashuhudia jamii ya mwanadamu ikipitia katika sintofahamu kubwa na kuanza kumtafuta mchawi ni nani?

Vijana wote wanaohangaika kutafuta ajira Tanzania na kwingineko duniani lengo lao kubwa ni kuwa na uhakika wa mahitaji hayo matatu, ama wenyewe wakijua au bila ya kujua.

Kwa bahati mbaya mfumo wa ajira rasm kwa Tanzania na nchi nyingine zinazoendelea unaweza kuhimili watu wachache tu, tena wachache hao (watumishi wa uma) wamekuwa wakifanya kazi kipindi kirefu cha maisha yao kwa ujira mdogo wa kuwawezesha kupata chakula, mavazi pamoja na kulipa kodi ya pango huku wakisubiri mafao ya kustaafu ili walau waweze kumiliki angalau nyumba.

Kuna raha gani kupata nyumba nzuri wakati umeshafika umri wa miaka sitini au unakaribia sitini? Labda habari njema kwa watoto ambao mtumishi amebahatika kuwapata kwani wao ndiyo watakuwa warithi wa hayo makazi.

Tuombe Mungu kwamba hiyo familia isiwe yenye migogoro kwani hako hako kajumba kanaweza kakawa sababu ya kuleta mtafaruku wa kifamilia, endapo aliyejenga akitangulia mbele za haki - sio jambo geni kwenye jamii yetu.

Kujiajiri (Ujasiliamali) Kama Suluhu Ya Changamoto Za Watanzania.

Kutokana na ongezeko kubwa la watu Tanzania na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa ajira rasmi, ujasiriamali umeonekana kuwa ndio njia sahihi na ya uhakika ya kutatua changamoto hiyo.

Kuna swali la kujiuliza hapa; je, ni kweli kwamba kujiajiri ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo ya Watanzania? Tukiweka pembeni suala la mitaji, tukichukulia kila Mtanzania amepewa milioni kumi ili afanye ujasiriamali.

Je, ni kweli kwamba jamii yetu itaimarika na kustaarabika baada ya kupata mitaji hiyo? Jibu ni hapana!

Kugawa mitaji mikubwa kwa watu wote wafanye ujasiliamali hakuwezi kumaliza matatizo ya jamii ya watanzania. Kuweka miongozo na misingi ya jamii iliyostaarabika ndio kitu kinachohitajika kwa sasa. Jamii nyingine zilishaliongelea swala la ustaarabu na nidhamu kwenye jamii zao kipindi kirefu nyuma. Kiasi kwamba sasa hivi wanaishi katika huo ustaarabu waliojiwekea. Ili kufika tunakotaka kwenda ni lazima kwanza tuanze kuweka picha vichwani mwetu. Picha ya jamii tunayotaka tuishi ndani yake kisha baada ya kupata hiyo picha ndio tuanze kutafuta njia zitakazotufikisha tunakokutaka. Kwa kufuata njia ambazo tutakuwa tumejiwekea tutafika mahala tunataka tuwepo.


Umuhimu Wa Pesa Kwenye Maendeleo Ya Watanzania

Ni vema kwanza kuelewa nadharia nzima ya fedha na umuhimu wake kwenye ustawi wa jamii ya watanzania. Hii ni kwa sababu mawazo ya jamii nzima yapo katika kutafuta pesa, kitu ambacho kimefanya pesa kupewa kipaumbele cha kwanza karibu na kila binadamu wa karne hii. Lakini je, kweli mtazamo huu tuliokuwa nao kuhusu fedha ni sahihi?

Maulid Siogopi
0753887199.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom