SoC02 Jiwe La Msingi 3. Ukombozi Wa Fikra, Elimu na Uchumi

Stories of Change - 2022 Competition

onea 22

Member
Joined
Jul 31, 2020
Posts
34
Reaction score
20
tunaendelea kutoka thread namba 2.

Pesa ni mfano mmojawapo mzuri wa nadhaharia inayoitwa “Tinkerbell effect”. Ambayo inajaribu kuelezea kwamba baadhi ya vitu vipo kwa sababu tu ya watu kuamini vitu hivyo. Watu wengi wanavyozidi kuamini kuwa pesa ina thamani sana na hakuna maisha bila pesa basi ndo inakuwa kweli.

Sasa tujaribu kuangalia japo kwa mfano mdogo tu mizunguko ya pesa kwenye jamii ya watanzania. Walanguzi (wajasiriamali) wamekuwa wakikusanya vyakula kutoka kwa wakulima kwa bei ya chini sana na kwenda kuviuza mijini kwa wafanyakazi wa serikalini, viwandani na wafanyabiashara wengine.

Zoezi hili huwa ni la kujirudia kila mwaka. Wakulima ambao ni karibu asilimia themanini ya jamii nzima wanazalisha, uzalishaji ambao hauwawezeshi hata wao wenyewe kuwa na ziada ya chakula.

Chakula hichohicho kidogo wanachokizalisha ndicho kinauzwa mijini ambapo ndio kuna matumizi makubwa zaidi ya vyakula. Kwa uwezo na akili ya mwanadamu ukijumlisha na wingi wa idadi ya watu wanaojihusisha na kilimo (bila kusahau ukuaji mkubwa wa teknolojia), Tanzania ilitakiwa tuzalishe na tuweze kuhifadhi chakula hata cha miaka kumi mbele.

Lakini kitu cha kusikitisha ni kwamba ukitokea ukame mwaka mmoja tu, shida ambayo jamii ya Watanzania wanapitia ni kubwa sana (kumbuka mwaka 2017 ambapo kilo ya unga ilifikia T. Sh 2500 katika miji mingi ya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar).

Mawazo ya Watanzania wengi yamezama kwenye kutafuta fedha ili waweze kupata mahitaji yao ya muhimu. Matokeo yake mkazo mdogo unawekwa kwenye uzalishaji wa chakula huku zana duni na mbinu zilizopitwa na wakati zikitumika.

Ukweli ambao Watanzania wengi hawaufahamu ni kwamba sisi binadamu hatuhitajii fedha ili tuweze kuishi. Mahitaji halisi ya mwanadamu yeyote ni chakula, mavazi na malazi kama tulivyoainisha huko nyuma.

Kwa jamii ambayo iko makini inaweza kujiwekea mifumo madhubuti ya kuwawezesha kujipatia mahitaji yao ya msingi bila ya kuhitaji kuwa na fedha (ninaamini kila jamii ina uwezo wa kufanya hivyo).

Fedha ni kitu ambacho kimetengenezwa (kinatengenezwa) na kikundi cha watu wavivu wasiotaka kufanya kazi. Kwa kutumia akili nyingi wanataka kuwafanyisha watu kazi kwa kuwalaghai kwa hizo fedha zao ili wao waishi kama watawala duniani.

Kwa hiyo wametengeneza pesa kisha wakawaaminisha watu kwamba hawawezi kuishi bila ya kuwepo kwa hizo fedha.

Kwa kuwa wao ndio wanazitengeneza, ni wazi kwamba watakuwa nazo nyingi sana na watapata kila wanachokitaka kwa kutumia hizo karatasi zao. Sisi hatuzalishi hizo karatasi na tunahisi hatuwezi kuishi bila ya hizo, kwa hiyo tutafanyishwa kazi tofauti tofauti ili tupate hayo makaratasi. Na kibaya zaidi tunatoa mpaka mali zetu kwa thamani ya hizo karatasi tu.

• Unataka pesa? Nipe dhahabu nikupe pesa.

• Unataka pesa? Nipe pembe za ndovu...

• Unataka pesa? Nipe almasi...

Mara kadhaa mkoani Morogoro (hasa wakati wa mavuno) gunia la mahindi limekuwa likiuzwa kwa shilingi 40,000 au chini ya hapo. Swali la kujiuliza je, ni kweli noti tatu au nne zina thamani sawa na gunia la mahindi?

Hapana, kama tukifuata haki, mwenye hizo noti hatakiwi kupata hata robo tu ya gunia la mahindi. Ushahindi ni kwamba, tujaribu kuwatenga watu wawili hao mmoja na pesa zake na mwingine na chakula chake kisha tuone ni nani atakayeweza kuendelea kuishi.

Pesa ni janja tu ya baadhi ya watu ili waweze kuitawala dunia. Wanataka sisi wengine tuendelee kuwa wajinga siku zote, tuzalishe chakula kidogo kila siku ili tusiweze kuwa na akiba.

Kwa maana nyingine kila siku tuendelee kuwa wahitaji wa chakula na vitu vingine. Katika historia tunasoma kwamba moja kati ya sababu iliyopelekea kukua kwa Falme kubwa barani Afrika kabla kuja kwa wakoloni ilikuwa ni kuzalisha chakula kingi mpaka kuwa na ziada.

Cha ajabu ni kwamba, mbali na maendeleo makubwa ya teknolojia kipindi hiki bado Watanzania na watu wengine wengi wa dunia ya tatu wanashindwa kuwa na ziada ya chakula.

Mara nyingi tumekuwa tunasikia Wazungu wanatoa misaada ya fedha kwa nchi za Afrika. Lakini mimi binafsi sijawahi kusikia hao wafadhili wakitoa misaada ya vifaa kama matrekta kwa nchi kama Tanzania kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Labda gharama ya kununua trekta ni kubwa sana hivyo hao wahisani hawawezi kutoa. Lakini mbona mara nyingi nimekuwa nikisikia mamilioni ya dola yakitolewa kwa nchi za dunia ya tatu kama Tanzania?

Ukweli ni kwamba hao wanaojiita wahisani au wafadhili wanajua kuwa hatuhitaji hizo fedha ili tuweze kujikwamua kutoka katika hali tuliyo nayo na kuimarisha jamii yetu. Hizo fedha wanazotupatia sio kwamba wanatupa bure kama wengi wanavyodhani bali tutakuja kuwalipa.

Je, tutawalipa nini kipindi hicho ambacho hatunazo tena hizo fedha? Kumbuka pia kwamba sisi hatuwezi kufyatua hizo noti zao! Yawezekana ikawa ni rahisi kulipa hayo madeni tofauti na ninavyofikiria, tunauza madini yetu nje ya nchi ili tupate fedha za kigeni (makaratasi tena) ili tuweze kulipa madeni tunayodaiwa.

Lakini kitu kingine ambacho sio rahisi kueleweka kwa mtu mwenye kutafakari mambo ni kwamba kwa nini hiyo mikopo iliyokuja huko nyuma viongozi wetu wasingeielekeza kwenye kununua zana za uzalishaji pamoja na teknolojia kutoka nje ya nchi badala ya kuzileta hizo fedha ndani ya nchi na kufanyiwa matumizi mengine yasiyokuwa na tija kwa taifa?

Mpaka kufikia mwezi wa kumi mwaka 2017, deni la taifa lilikuwa likikadiriwa kuwa trilioni 50. Ni fedha kidogo ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki. Lakini tukijaribu kuulizana hizo fedha tulizokopa zimeacha alama gani kwenye maendeleo ya taifa, tutabaki kuangaliana tu.

Hofu nyingine inayotia shaka ni kwamba baada ya fedha kuwa ngumu zaidi kupatikana, itawabidi wanadamu wengi zaidi wajifunze kutengeneza fedha zao wenyewe ili waweze kumudu gharama za maisha.

Ni kipindi hiki tu kesi za kukamata watu na mitambo ya kufyatulia noti bandia zimepungua, lakini sio kweli kwamba watu wenye taaluma hiyo wamepotea kabisa nchini Tanzania na duniani kote.

Inawezekana pia teknolojia yao imekuwa kiasi cha kushindwa tena kutofautisha noti feki na halali. Pale ambapo noti zitakaposambaa kwa kiasi kikubwa ulimwenguni, ndipo watu watakapotambua kwamba hayo makaratasi si chochote si lolote.

Siku tukija kufika huko njia ya kubadilishana bidhaa itabidi ibadilike kutoka kwenye fedha na kuhamia kwenye vitu ambavyo havitengenezeki kirahisi kwa akili ya mwanadamu, vitu kama dhahabu, fedha, almasi na madini mengineyo.

Pia ni wazi kwamba watu wa dunia ya kwanza wanalijua hilo na wanajiandaa kwalo. Muda ambapo Waafrika na watu wengine wa dunia ya tatu wanakuja kuamka, sehemu kubwa ya dhahabu na madini mengine yatakuwa yamehamia Ulaya.

Hapo ndipo mambo yatakapobadilika kwani Waafrika wa wakati huo itawabidi kuwatumikia tena Wazungu kwa malipo ya vitu kama dhahabu, fedha na madini mengine. Wakati huo wajukuu zetu watakuwa wanayaangalia mashimo yaliyobakia huko Buzwagi, Geita, Bulyanhulu n.k kama makumbusho tu kwamba walikuwaga na mali zamani.

Watakuwa wanajiuliza sisi wazee wao tulikuwa wapi wakati wenzetu walipokuwa wanahamisha utajiri wote na kuupeleka kwao? Niwajibu tu kwamba kwa sasa tumeshughulishwa zaidi na mambo ya michezo na burudani, kwamba hizo changamoto ni nzito sana kwetu hatuwezi kupambana au kwenda kinyume na ngozi nyeupe.

maulid siogopi
0753887199.
 
Upvote 1

Thread zako zote nzuri ndugu! Na nimekupigia kura! Twende pamoja.
 
Back
Top Bottom