Jiwe la msingi SGR Mwanza - Isaka kuwekwa hivi karibuni, ujenzi kuanza punde si punde

Jiwe la msingi SGR Mwanza - Isaka kuwekwa hivi karibuni, ujenzi kuanza punde si punde

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Maandalizi kwa ajiri ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Sgr kati ya Mwanza na Isaka yamekamilika. Na jiwe la msingi litawekwa wakati wowote na rais wa JMT, SSH.

Ziara ya kukagua maandalizi hayo imefanywa na waziri wa ujenzi Leonard Chamuriho akiwa na naibu wake Mwita Mwikabe na maandalizi kwa ajiri ya uzinduzi wa ujenzi yamekamilika.

Hii itakuwa ni nafasi ya watanzania kupima kampuni ipi ipo faster kukamilisha ujenzi wa reli hii ya Sgr kadri ilivyopewa kandarasi maana kampuni ya kituruki ya Yapi Merkezi inachechemea zaidi ya miaka minne kukamilishsa kipande cha Dar mpaka Moro.

IMG_20210404_163712.jpg
 
Rais aachane na iyo kwanza...hiyo hela ya kipande hicho imwagwe mtaani mzunguko wa hela uwepo mjini
 
Huo ujenzi utakamilika lini ili mambo mengine ya maisha yaendelee?
 
Kipande cha Isaka Rwanda ndio kingepewa kipaumbele kwani hiyo milima kuipasua sio mchezo kwa spidi hii itachukua maalfu ya miaka hadi kufika Kigali
 
Kipande cha Morogoro - Dodoma - Singida kina changamoto za kijiographia, Bonde la Ufa, Mito mikorofi kuchelewa ni kawaida ila hiki kipande cha Mwanza - Kahama hakina mziki mkubwa. Pia Isaka - Rusumo kuna shughuli milima ya kuchoronga ni mingi sana nacho kitachukua muda
 
Isaka - Rusumo lini?
 
Back
Top Bottom