Jizuie: Kati ya vifo 5, vitatu(3), chanzo ni kula vibaya

clion dismas

Senior Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
185
Reaction score
169
Habari ndugu zangu, poleni na majukumu ya hapa na pale naamini MUNGU ni mwema kwa kila jambo, HEBU TUHABARISHANE NA TUELIMISHANE KIDOGO KATIKA MASWALA YA LISHE NA VIFO.

Kabla ya yote yale, tunaamini ya kwamba MUNGU ndiye aliyetuumba na ndiye alituagiza tule nini kabla ya anguko la mwanadamu. Ukisoma kitabu cha biblia, mwanzo 1:29 utayakuta maagizo ya MUNGU kuhusu chakula kitupasacho.

"TIZAMA, NIMEWAPA KILA MCHE UTOAO MBEGU ULIO KATIKA USO WA DUNIA NA KILA MTI UZAAO MATUNDA YENYE MBEGU NDANI YAKE, MTAVITUMIA KAMA CHAKULA" (mwanzo 1:29)

Ndugu yangu, ingia katika tafiti nyingi, scientific journals na reserchs nyingi zinzonyesha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yanaongezeka kwa kasi ya kutisha na hakika ndiyo yanaongoza kwa kukatiza maisha yetu leo hii duniani.

magonjwa ya kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya saratani , magonjwa ya macho, magonjwa ya moyo na mengineyo, yamekua yakiongezeka kwa kasi kubwa. na pia, magonjwa kama haya ndiyo vifo vyake vinaripotiwa kwa wingi sana.

Naam, vifo 2 vinavyobakia kati ya 5 vimehusishwa na ajali za barabarani na nyingine kwa ujumla na nyingine ni maradhi ya kawaida ya kuambukizwa.

AJABU NI HII. VITUO VINGI VYA TIBA MBADALA VIMESHAMIRI DUNIANI LEO HII, WANATUMIA VYAKULA NA MATUNDA KATIKA KUTIBU MAGONJWA HAYA KAMA UIYAWAHI MAPEMA. TENE, WANAYATIBU KWA GHARAMA KUBWA SANA.

NIMSHUHUDIE MAMA YANGU, KAZUNGUKA HOSIPTALI NYINGI KUBWA HAPA MJINI, LAKINI HAKUPATA AFUENI YOYOTE. KITU KILICHOMTIBU NI MATUNDA, NDIO, MATUNDA NA MBOGAMBOGA NA NAFAKA NZIMA.

Tiba mbadala, wnafuata agizo la MUNGU, chakula ni matunda na nafaka nzima ndugu zangu.
JITATHMINI KIDOGO, KILE KINACHOKUSUMBUA, UKIENDA HOSIPTALINI, UNAAMBIWA JAMBO GANI? 1. TUMIA NAFAKA NZIMA, 2. TUMIA MATUNDA MENGI NA 3. TUMIA MBOGAMBOGA.

KWANINI UNGOJE MPAKA UAMBIWE? ANZA KUISHI MAISHA YA FURAHA, MAISHA YA NAFAKA NZIMA, MATUNDA NA MBOGAMBOGA, MUNGU NA AKUBARIKI SANA.

KWA KIFUPI, WAWEZA FUATA HII LINK KUTAZAMA VIDEO NILIYOELEZEA HAYA YOTE KWA UFUPI ZAIDI.


 
Kwa uzoefu wangu vyakula vya wanga tena vilivyokobolewa ni hatari Kwa mlaji yoyote,najaribu kuwaza kama watu tungeishi Kwa kula mbogamboga na matunda kiasi na vyakula visivyokobolewa kabisa na kuepuka kula usiku wakati wa kulala ,hospital wateja wangepungua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
well said beloved, be blessed much, let us shout to our maximum as long as GOD still hold our breath of life
 
Je unywaji wa maji una nafasi gani katika uzima wa miili yetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
maji ni kitu kikubwa sana kwenye miili yetu. mfano, unywaji wa water therapy lita 1 na nusu ndani ya muda wa dakika 1 hadi 3 kila siku mapema asubuhi, unasaidia kuflash system yako ya mwili kwakuondoa mabaki ya vyakula mwilini kwa njia ya haja ndogo.
 
tangu jana nalijibu, ila sielewi, iko pending, yasubiri approval.
hebu soma hii pdf, sehemu ya kitabu changu( TIBA MAJI)
 

Attachments

maji ni kitu kikubwa sana kwenye miili yetu. mfano, unywaji wa water therapy lita 1 na nusu ndani ya muda wa dakika 1 hadi 3 kila siku mapema asubuhi, unasaidia kuflash system yako ya mwili kwakuondoa mabaki ya vyakula mwilini kwa njia ya haja ndogo.

Ndugu shukrani kwa mchango wako, niboreshe kidogo . Kama mtu hajazoea tumia maji kama tiba, sitomshauri kuyatumia mara moja kiasi hiko chote.

nimerejea tafiti nyingi na hakika bado zinaendelea, tafiti nyingi zimeonesha utumiaji wa maji mengi kwa wakati mmoja bila ya mwili kuzoea kuna uwezo wa " cell swelling", yaani tuseme sijui namna gani kwa kiswahili, ila ni hali ya seli za mwili wa binadamu kuweza kama vile kupukutika/kupoteza umbo asilia/kuyeyuka(kiswahili kizuri mtusaidie hapa) kwa kupoteza madini muhimu kama potashi na sodiamu kwa sababu ya kuzidiwa na maji mengi. na kwa ufupi, yapelekea matatizo mengi sana. shida kama kukojoa sana, kichefuchefu na kutapika yameripotiwa maeneo kadhaa na hadi vifo.

Ni vyema ikafuatwa kwa maelekezo ya mtaalamu wako wa afya kabla ya kuanza kutumia maji hayo, ZAIDI , REJEA HII PDF, SEHEMU YA KITABU CHANGU, " MUNGU NA UPONYAJI KATIKA MATUNDA, NAFAKA NA MBOGAMBOGA"- ISBN 978-9976-5087-0-3
CLION O DISMAS

BE BLESSED
 

Attachments

Siku hizi angalau jamii imeanza kuelewa... ukienda mgahawani(kwetu uswahilini) na ukaagiza ugali samaki,utaletewa ugali wa dona na huyo samaki.

Ukishangaa kwa nini wameleta dona badala ya sembe nawe watakushangaa maana siku hizi ukisema ugali maana yake ni wa dona, hivyo ukitaka ugali wako wa sembe(makapi yasiyo na kitu) inakupasa kusema mapema 'nileteeni wa sembe'.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…