Ila Kama polisi wangekuja na virungu vyao na kumfukuzia mbali Rais wakati akihutubia mkutano ingekuwa hatari! Maasi!
Lakini hakuna sababu Lewis Makame ashindwe kukemea ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.
Vile vile, sijajua ni kwa nini Jaji Mkuu hajathubutu kukemea kitendo cha Rais kusema kesi ya Mramba ni ndogo tu, na atashinda. Mahakama ni nguzo mojawapo ya serikali. Nguzo ya Utendaji ikivuruga sheria inabidi ikanywe. Mheshimiwa Ramadhani, timiza wajibu wako wa kikatiba. Taifa linasubiri lisikie utasemaje.