Jaji Mkuu Mstaafa Barnabas Samatta ateuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe
JK amemteua Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Albert Samatta (pichani) kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuanzia tarehe 13 Mwezi wa Kwanza 2009.
Kwa mujibu wa taarifa ilyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Hamis Dihenga imesema Uteuzi huo wa Jaji Mstaafu Samatta umekuja baada ya aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Balozi Dokta Ibrahim Kaduma kumaliza kipindi chake cha uongozi.
Wakati huo huo Rais Kikwete amemteua Balozi Nicholas Alfred Kuhanga kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kipindi kingine cha miaka minne kuanzia tarehe 1 mwezi wa 11 mwaka 2008.
Aidha Profesa Idris Kikula ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kipindi cha miaka minne kuanzia tarehe 29 mwezi wa kwanza mwaka huu kufuatia Profesa Issa Omari kumaliza kipindi chake cha Uongozi
Source: MICHUZI