JK afanya teuzi tatu

Mfumwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2008
Posts
1,455
Reaction score
42
Jaji Mkuu Mstaafa Barnabas Samatta ateuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe
JK amemteua Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Albert Samatta (pichani) kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuanzia tarehe 13 Mwezi wa Kwanza 2009.

Kwa mujibu wa taarifa ilyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Hamis Dihenga imesema Uteuzi huo wa Jaji Mstaafu Samatta umekuja baada ya aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Balozi Dokta Ibrahim Kaduma kumaliza kipindi chake cha uongozi.

Wakati huo huo Rais Kikwete amemteua Balozi Nicholas Alfred Kuhanga kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kipindi kingine cha miaka minne kuanzia tarehe 1 mwezi wa 11 mwaka 2008.

Aidha Profesa Idris Kikula ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kipindi cha miaka minne kuanzia tarehe 29 mwezi wa kwanza mwaka huu kufuatia Profesa Issa Omari kumaliza kipindi chake cha Uongozi
Source: MICHUZI
 
Kwa nn tapendelea wastaafu.Kwani hamna wengine ambao bado wanaweza kuja na vitu vipya badala ya kuendeleza vicious circle ?
 
Pia amefanya uteuzi wa wajumbe wa bodi mbalimbali za mashirika/makampuni ya umma - wamo Abdallah Kigoda na Maria Kejo (Tazama orodha kamili kwenye The Guardian)
 
bongo kweli kazi.
sasa kusiwe na umri wa kustaafu utumishi wa uma basi.
 
Kwa nn tapendelea wastaafu.Kwani hamna wengine ambao bado wanaweza kuja na vitu vipya badala ya kuendeleza vicious circle ?

Tz ndio kwanza tunaanza kusimika SS kwa msaada wa PSI ya IMF; toka enzi za JKN hizo kazi za ujumbe wa Bodi za mashirika ya UMMA ndio SS ya wakuu wetu - ndio pensheni hiyo kutoka kwa JK!
 
CCM waondoke madarakani hii si nchi yao wala wao sio wenye hati miliki,mijitu imeshafanya kazi tokea tupate uhuru bado imeng'ang'ani ,maana yake ni nini ?
Watu kibao wamemaliza Chuo kikuu na vyuo vyingine vya nchi za nje lakini hawapewi uongozi hata wa ualimu mkuu maana yake ni nini na badala yake tunaona zile zile sura za kufa zikikabidhiwa mikoba ,hivi kuna kosa gani ikiwa vizazi vipya vitakabidhiwa mamlaka na hizo sura za kufa kuwa washauri tu pale panapohitajika ushauri.
CCM mtaondoka tu mkitaka msitake.
 

Hivi wajameni,

Mwataka kuniambia wazee hawatakiwi kabisa kwenye utawala wa taifa letu... mtu kama jaji mkuu mstaafu... kichwa bado kinafanya kazi... lakini pamoja na hayo... hiyo kazi ya mkuu wa chuo... sio nzito kiasi kwamba hawezi... kwani sio kazi ya kupiga matofali ya block.

Mtu kama jaji mkuu, mkuu wa majeshi etc... they have to have things to do to keep them busy...

Alafu waheshimiwa, kwa mtu aliyetunzwa vizuri na kuishi vizuri kama jaji mkuu, bado anatakiwa atumikie taifa.
 
bongo kweli kazi.
sasa kusiwe na umri wa kustaafu utumishi wa uma basi.

Wenzako wanataka wazoefu wa muda mrefu, wewe huwataki.!!! hata wale wenye "uzoefu kama mwaka mmoja" tu hao hawatakiwi..basi kazi kwelikweli...!!!
 
..kazi kama za Ukuu wa Vyuo Vikuu huwa wanapeta watu wenye uzoefu wa muda mrefu sana, au wastaafu. kazi hizi huwa ni ceremonial zaidi.

..nadhani kwenye ukuu wa idara ndipo panapotakiwa watu mchanganyiko -- wenye uzoefu, na wale wenye mawazo mapya.
 
Pia amefanya uteuzi wa wajumbe wa bodi mbalimbali za mashirika/makampuni ya umma - wamo Abdallah Kigoda na Maria Kejo (Tazama orodha kamili kwenye The Guardian)

Mkuu Companero asante kwa ujumbe, sahihisho dogo, nadhani Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi Wakuu huteuliwa na Rais, ila wajumbe wa bodi huteuliwa na Waziri ambaye shirika/kampuni ya umma iko chini yake. Mfano Rais anamteua mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda –TIRDO, na waziri wa Viwanda na masoko anawateua wajumbe wa bodi hiyo ya TIRDO.
 
Kustaafu ni heshima kubwa kwa mtumishi yeyote hasa wa UMMA.
Kikwete anapo teuwa wastaafu kushika nyadhifa,je pensheni ya mtaafu itakoma mara moja au atachukua pensheni huku anapokea mshahara?Je kama anaendelea kupokea vyote akistaafu tena kwenye kazi mpy atapokea pensheni nyingine?
KAMA ANAPOKEA PENSHENI HUKU ANAFANYAKAZI,HII KUWANYIMA 'VIJANA' Wenye uwezo nafasi za ajira
 
..Raisi anateua lini Mabalozi?

..nimesikia kuwa, Balozi Mtango wa Japan, na Balozi Mwambulukutu wa South Africa, wamestaafu.
 
jamani kipyi kipya!!!huyu muungwana ni wa kuzoe tu ameshachoka na nchi hii#

eg: MATTAKA+NIC/ JK = ATCL

JAMANI KABAKZA KUMCHAGUA MKEWE TU!!
 
Kitu kinachonishangaza katika serikali ya Kikwete ni pale waziri wake anapoliambia bunge kuwa sio utawala bora kwa wabunge kuwa wakurugenzi wa mashirika ya umma kwani wana compromise independent oversight function ya bunge juu ya vyombo hivyo!! Hapo hapo Rais anawateuwa wabunge kuwa wenyeviti wa bodi za Tumbaku ,Pareto na Mkullo nae anawajaza wabunge kwenye bodi zote za benki; cheki list yake aliyotoa wiki hii utaona ;Kigoda, Kaboyonga, Msindai,Nyami, Kilasi,Likokola, Mayenga, Ndassa etc.Mpaka ameteua hata mmoja wa wajumbe aliyekuwa bodi ya BOT wakati wanakwapua fedha za EPA!! Hawa jamaa mbona sio makini nadhani tunapigia gita mbuzi!!!! Serikali inatakiwa iwe mfano wa yale wanayotuambia.
 
Last edited:
Jamani hapo kuna TECHNICAL KNOWHOW!...........au vp?mimi naona sawa tu,kama mtu haridhiki na hilo APENDEKEZE majina yeye basi.

............watu wengi tuna notion ya KULAUMU TU,KULAUMU TU.

mimi naona tuwe tunaonyesha appreciations sometimes eeh jamani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…