Huyu Dada ni huyu hapa cheki maelezo yenye bold...
RAIS Jakaya Kikwete amewateua wanawake watatu kuwa maafisa katika ofisi yake binafsi. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyopatikana jana, walioteuliwa ni Elsie Kanza kuwa msaidizi wa Rais wa Mambo ya Uchumi, Fatma Mwasa kuwa Msaidizi wa Rais wa Masuala ya Jamii na Premiere Kibanga kuwa Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi. Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kibanga atakuwa akishirikiana na Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi wa sasa, Maura Mwingira.
Kabla ya uteuzi huo, Kanza alikuwa msaidizi maalumu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Mwasa alikuwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS na Kibanga alikuwa Afisa Habari wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) Kusini mwa Sudan . Taarifa inaeleza kuwa usteuzi huo unaanza mara moja