Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Jk akitegemea historia kujirudia yenyewe alitarajia awamu ya pili itakuwa mteremko lakini siasa huwa hazitabiriki kabisa.
Kinyume na matarajio yake amekutana na ghadhabu ya wapigakura wenye kiu ya kupata kiongozi makini sifa ambayo bahati mbaya sana hana..
JK anafikiri uongozi ni kutukenulia meno yake ya bandia yaani "veneer teeth" lakini wapigakura wamemwonyesha ya kuwa uongozi si swala la sura ila ni la kuwa na uwezo wa kuwatumikia wananchi kwa unyenyekevu usio na mipaka...
Sasa JK amepigwa na butwaa na hata ahadi zake lukuki wapigakura hawana imani nazo na swali wanalojiuliza ni kuwa ni kitu gani atakifanya ambacho miaka mitano iliyopita hakukifanya?
Ni nini kilimzuia hayo yote anayoyaahidi sasa kutoyafanya hata theluthi moja kipindi chake cha kwanza.........
JK yupo kimya juu ya vita vya ufisadi na misamaha ya kodi kutoka kwa wakubwa sasa hizo fedha atazitoa wapi?
JK anawategema wamarekani ndiyo kutuletea maendeleo kweli hio ni sahihi? Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe wafadhili kazi yao ni kuongeza chachu tu na wla siyo vinginevyo................
JK hayupo tayari kuongelea ahadi zake zitaligharimu taifa kiasi gani ili kuona ya kuwa kweli yuko makini na anachoongea.................Ukweli ni kuwa anajitamkia tu ili kuwarubuni wapigakura tu................
Safari hii, JK atawafahamu watanzania kuwa siyo watu wa kuwachezea chezea kama watoto wadogo na kututishia na JWTZ amechochea petroli kwenye chaguzi hii... Vitisho vya JWTZ kamwe havitaweza hata siku moja kutumika kutuchagulia kiongozi tusiyemhitaji................
Hamu ya wapigakura kumfunza adabu inaongezeka siku hadi siku na katika kipindi cha wiki mbili tutatoa hitimisho lake bila huruma hata chembe.............