<br />
<br />
Amen! Mungu ashukuriwe kuwa ameamua kutukomboa mwenyewe! Mungu karibu Tanzania uisafishe nchi hii, tumeonewa vya kutosha, vunja kila miungu inayoabudiwa kinyume chako, wakomeshe watawala wanaotusababishia maisha magumu hadi wengine tunakikosea kwa kulazimishwa! Wachukue utumwani watawala wetu kama ulivyomchukua mfalme Nebkadreza porini miaka saba! Hiyo iwe kwa wale unaotaka wajirekebishe, lakini kwa wengine waondolee mbali pamoja na uzao wao kama Ahabu na Sauli! Najua kila aliyemtumainia mchawi akakuacha wewe utamshughulikia kikamilifu na haitakuwa kwa sauli na Ahabu tu, tunataka kukuona ktk hili ili tuamini maneno yako kuwa yaliyoandikwa kutendeka yalitendeka kweli na ni wewe yuleyule jana, leo na hata milele.
Nakushukuru Mungu kwa kusikia maombi yangu kwa niaba ya WaTanzania wote
wanaoteseka na kuonewa na jina lako na watumishi wako kutukanwa!