Wadau, kama Dr. Slaa au chadema wanawaza ku-include mtu yeyote wa chichiem kwenye cabinet yake ninamwomba sana aache wazo hilo kabisa. Watanzania wapo wengi mno wanaoweza kuongoza na wanaotoka nje ya wigo wa mafisadi. Kuna anasema jk apewe sijui uwaziri wa nini sijui. Kwangu mimi, jk anafaa ajiendeshee NGO yake itakayokuwa inashughulika na umbaji wa misaada nchi za nje. Zipo kazi nyingi tu zinamfaa kama vile ujaji wa Miss Ilala, Kinondoni na Temeke. Anaweza pia akajaza nafasi ya Kaijage pale TFF.