Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
Nimekuwa nikitafakari jinsi Marais wanapokuwa madarakani katika ungwe ya awamu ya miaka mitano ya mwisho ya uongozi wao, mara kadhaa Marais hao kwa kuwa hawana tena cha kupoteza hubadilika sana. Labda nianze na awamu ya pili ya Mzee Ruksa. Huyu alitaka kuiuza Nchi kwa Waarabu kwa kuitumbukiza kwenye Jumuiya ya OIC kinyemela bila hata ya Bunge kuwa na habari, kisa mafuta na udini! Ameshiriki sana kuuza utajiri wetu kwa Waarabu kupitia kashfa ya Loliondo. Mambo yote haya yalitokea kwenye kipindi cha Pili cha uongozi wake!
Mzee Mkapa alijulikana sana kama Mr "Clean" kwenye awamu ya kwanza ya uongozi wake, lakini mambo yalibadilika sana katika awamu ya pili. Aligeuka kuwa fisadi la kutisha!
Mambo haya labda yanafanyika kipindi hiki kwa sababu hawa waheshimiwa hawakuwa na cha kupoteza katika ungwe ya pili ya uongozi wao.
Kwa upande wa JK alianza vizuri sana na wengi walimpa sifa mbalimbali km: "Tumaini lililorejea, chaguo la Mungu, nk" Mimi kwa upande wangu hata hivyo, kusema ukweli toka moyoni, sijaona matunda ya JK ya kuwaletea maisha bora kwa kila m-TZ kama alivyoahidi. Wala sikutegemea kama angeleta maisha bora kwa kila m-TZ! Amekuwa mtu wa safari nyingi za Marekani, sijui ya sasa ni ya ngapi na sijui ameteketeza mabilioni mangapi kwa safari hizo! Sijui vile vile kama atafuata nyayo za akina Mzee Ruksa na Mzee Ben za kutokujali zaidi katika ungwe ya pili ya uongozi! Let's wait n c!
Nakaribisha mjadala!