Elections 2010 JK auza nchi kwa magaidi?

hahaaa kazi kweli kweli JF siku hizi imekuwa kama baraza za kahawa pale kariakoo na magomeni.


....wana JF katika hatua tuliyofikia hatutakiwi kudharau taarifa hata moja...uzoefu wangu unanionyesha kuwa kwenye data collection and analysis hata taarifa inayoweza kuonekana ni ya kijinga ....ukiunganisha dots unaweza kuibuka na utambuzi wa maana kabisa....

....mara nyingi informers kwenye maneno elfu moja ....anaweza kuwa amepatia kwa usahihi hata maneno MIA ....Kwa mfano taarifa aliyoleta mdau....ina ukweli ufuatao....

1] ni kweli marekani wameshamdaka rais wetu kifikra..........na ni kweli wana kawaida ya kumfanya rais wanayemdaka ajione hayupo salama bila ulinzi wao....

2] ni kweli watapenda utawala wake uendelee au ikibidi wawe na uwezo wa kutupangia viongozi au ikishindikana wasababishe machafuko tutawaliwe kijeshi na maafisa au viongozi watakaotaka wao,,,..

3]ni kweli ndani ya taasisi za kiusalama kuna watendaji na askari au field men ambao hawapendi hali ya nchi ilivyo.....

4] ni kweli kuna idadi kubwa ya NGO za kimarekani au zenye mkono wa kimarekani ........na nimeshapatwa kuambiwa na afisa usalama mmoja wa nchi moja[sio marekani]....kuwa tuwaeleze watu wetu wajiadhari na ongezeko la mashirika ya misaada ya aina hiyo........kwani mara nyingi huwa mission advance team kwa niaba ya CIA ,,,.....wanapojiandaa ku take over influence mahali..

5]Ni kweli mbega huponzwa na uuzuri wake ...UGUNDUZI WA URANIUM nzuri kabisa duniani...unawakosesha raha marekani hasa ukizingatia uhusiano wetu na china ...wanaogopa itawaponyoka...they one to make sure no one gets near.....thats possible by destruction ili wabaki kulinda amani hapa..

6] NI ukweli kuwa muasisis wa taifa letu alishaonya vyombo vyetu vya usalama hususani JWTZ ....Kutokuwa pro - AMERICANS ....kwani marekani ni maarufu kwa destabilization.......na wana sifa kuu ya kuwatumia viongozi kama big G....kwa mfano they are interms with JK for certain reasons now ..siku wakiona hawasaidii tena au mtandao wake hauwasaidii basi watamtoa wenyewe ..na italeta fujo...MAJEMEDARI WA ZAMANI WANALIJUWA HILI.......


sasa kuhusu hoja iliyombele yetu inawezekana kabisa kuna yaliyoongelewa ikawa porojo lakini kamwe haiondoi ukweli hapo juu...narudia lazima tusidharau information yeyote na dawa mwenye uwezo wa kufikisha hizi data kokote ni bora....siku hizi ni bora kufanya kazi na wachina na warusi kuliko yankees.....so dawa ni kuwagonganisha mapema ili wazuiane wenyewe kutudhuru......wakishaingia wakitaka kufungiana milango tutaumia sisi........
 
historia inaonyesha kwamba hakuna aliyewahi kufanya dili na wamrekani akafanikiwa... kaa ni kweli, basi watamtumia, kisha watammaliza, hakuna haja ya kurejea ni nchi gani watu wameangamia

jambo moja kuu zaidi ni kwamba upeo wa kiongozi mkuu wa nchi ni muhimu sana kung'amua nani ni rafiki na nani ni adui... PIA KUNA HAJA YA RAIS WETU KUANZA KUSOMA UPYA VITABU VYA HISTORIA NA MAPINDUZI YA WANYONGE, NAHISI AMESAHAU AU HAJAWAHI KUSOMA VITABU HIVYO

YOU CAN NEVER BE A GOOD PRESIDENT WITHOUT KNOWING YOUR HISTORY
 
Unatania? Rais wetu asome vitabu vya historia? Huo muda atautoa wapi? Hawa wote walimwona Nyerere zezeta na sasa wanajaribu kupindisha misingi aliyoiweka.
 
Unatania? Rais wetu asome vitabu vya historia? Huo muda atautoa wapi? Hawa wote walimwona Nyerere zezeta na sasa wanajaribu kupindisha misingi aliyoiweka.
then we are very unlucky
 
Bora nusu shari kuliko shari kamili, Dr Slaa for presidency on october 31. JK anasema mnaona sasa Obama ameahidi ataendelea kutusaidia tanzania, Jk anafurahi kweli kupeewa misaada. Its crazy you know. Jk toka ikulu huiwezi.
 

Hii habari ni fabrication na inalenga upinzani ukichukua nchi uongozi huo uanze kuwa na chuki na USA bila sababu za msingi, wala habari hii isitumike kwenye campaign itaharibu kuliko kujenga
 
jamani lisemwalo lipo, kama halipo basi li mlangoni laja.....!!! We can treat this info as a thinner cog in a large mashine... But it seldomly bring some unbreakable violency in our country! Ninacho amini mimi kwa mtu mwenye uelewa mdogo kama JK kucorrude na wamarekani ili tu apate kitumbua na kubaki ikulu ni rahisi sana
 
Kumbuka pia wamewekeza sana kujenga jumba lao la ubalozi hapo ujue kuna malengo ya muda mrefu .Msipuuze taarifa ifikishwe kwa wahusika
 
Nchi hiyo kubwa yenye kuhitaji uranium ni Marekani lakini marekani siyo kweli wanapenda vita ziwepo nchi za wengine. Huu uchambuzi una walakini sana. Hoja za kutoyachakachua matokeo ndicho USA wanataka na wanelewa yoyote atakayekuja watafanya naye kazi. Hii siyo nchi ya kislamu na hivyo kufurahia vita vya wenyewe kwa wenyewe na kauli kama hizi zilizochanganywa na ukweli huu zinalenga kutupofua macho:-

 
UWT watusaidie sasa, wanaweza kutusaidia. Uzalendo utumike kuokoa nchi. Taarifa ni za kweli, zifanyiwe kazi. Niko serious ile mbaya
 
Hii taarifa ni ngumu kuiamini. Mambo yaliyozungumziwa humu ni nyeti sana. Nahofia labda mwandishi kaunga matukio yanayoendana na ukweli na kutuletea. Labda tusubiri.
 
..... USA...... majasusi wakutupwa. Safari za kivasco dagama zitatuletea maafa. huyu jamaa hafai ataokota na kisichookoteka. baada ya danganya toto ya vyandarua sasa vita. hafai kabisa huyu...
 
Tunawez akuona kama porojo... well, kila mtu ana haki yake kimsingi katika kutoa fikra zake. Ukisoma kwa makini yaliyoandikwa katika kila mstari ni facts; na ni characteristics features za Americans. Americans has never had a friend in deed, may be Israel. Nao ni marafiki wa nie nikupe tu!!

Kwa akili za JK yeye anaona ni sawa! JK anajulikana, ni mbishi, haambiliki, ana visasi etc, kwa hiyo hata akishauriwa (kwani naamini lazima anashauriwa kabla ya kuamua) hasikii. Kwa haya naona yapo na si ya kudharau.

Hii nchi ni tajiri sana!!! Wazungu wanapenda utawala mbovu uendelee kuwepo kuwafaidisha wao....

Tumuweke tu DR. Slaa... just for changes.
 

Amini , usiamini, Bush hakuwa mjinga kukaa Tanzania siku nne bila malengo ya muda mrefu. Marekani hawawezi kumpenda Slaa kwani wanajua hawezi kurubuniwa kwa kutembelea ikulu ya Marekani. Wanapenda mtu dhaifu ili wamtumie kwa maslahi yao. Ila kwa hilo la vita vya wenyewe kwa wenyewe nalikataa, Marekani haiwezi shabikia hilo.
Hata hivyo, wasiwasi wangu ni kwamba, kama kweli Marekani wamekuja kumsaidia JK, basi hawataruhusu uchakachuaji wa kumpa ushindi wa kishindo, bali watampa kura ambazo zitaonyesha kwamba hawezi kutawala peke yake bila kushirikisha upinzani. Hilo likitokea , basi ni la kheri, kwani utakuwa mwanzo wa kupata katiba mpya na kkuzuia genge la wahuni waliomzunguka JK
 
This could be a hypothetical scenario, however, there is a possibility of this happening. My worry is how each sector takes this story. Watu nanaweza kuanza kufukuza vivuli vyao na hiyo ikaanza hayo matatizo yanayotarajiwa. Cha muhimu ni kila mTZ mwema kuichukulia kwa uangalifu sana.

Inawezekana ikawa hakuna hiyo "conspiracy theory" na hii ikaanzisha wanachokitaka kwa kuwachanganya wote, mtu asimuamini mtu, kitengo kisiamini kingine, etc.

Tuwe macho, na tuombe Mungu
 

KWa taarifa yako wamarekani wanatengeneza silaha kila kukicha; hawana pa kuuza wala pa kufanyia majaribio ya kweli!!! Kalagha bhao!!! Hakuna watu wanafiki kama hao basi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…