JK awashauri wabunge kutembelea majimbo yao

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Posts
4,816
Reaction score
684
Hapa nakubaliana na mheshimiwa rais kuhusu utoro wa wabunge majimboni kwao.

Halmashauri nyingi zina matatizo makubwa ya capacity, viongozi wao wengi hawana uwezo. Wabunge ni katika watu wachache ambao wana uwezo na kama wangelikuwa wanashiriki ipasavyo kwenye mijadala ya hizo halmashauri wangesaidia sana. Lakini wengi wao wanashinda Dar na kwenye kamati, matokeo yake halamshauri nyingi utendaji wake mbovu sana.

Jukumu la kwanza la mbunge lazima liwe kuwahudumia watu wa jimbo lake na sio kushinda kwenye kamati mbalimbali akikusanya pesa za mahudhurio.

Pia pesa nyingi sana zinapotea kwenye halmashauri shauri ya kukosa uwezo na mipango mibovu. Wabunge waanze kusafisha majimbo yao kwanza kabla hata hawajafikiria kuibana serikali kuu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…