Elections 2010 JK: Elimu bure haiwezekani, ila kompyuta kwa kila mwanafunzi inawezekana

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
JK amekuwa akiwabeza wapinzani wake kuwa wanatoa ahadi ya kutolewa elimu bure wakati haitekelezeki. Lakini ni JK huyo huyo ambaye siku si nyingi alisema atatoa computer (desktop) kwa kila mwanafunzi nchini na laptop kwa kila mwalimu. Nadhani amesahau kwamba alichoahidi ni kigumu kutekelezeka kuliko wanachoahidi wenzake sasa. Kuweka computer kutahitaji computer set yenyewe, kiti na meza kwa ajili ya kuwekea computer (bila kujali kama kila mwanafunzi wa sasa anakalia dawati au la!), miundombinu km vile umeme kwa ajili ya kuendesha computer (sina hakika km aliwauliza TANESCO umeme umeishia wapi), solar panel zenye Watts za kutosha (iwapo hawatatumia umeme wa TANESCO, na sina uhakika kama aliuliza power consumption ya CRT desktop pekee), mafundi wa kuzifunga, maintanance costs na walimu wa kuwaelekeza wanafunzi walau namna ya kuzitumia.
Swali langu: Iwapo aliahidi computer + laptop, kwa nini awashangae wanaoahidi elimu bure? Kipi ni rahisi kutekelezeka, computer/laptop AU elimu bure?
Gharama ya jumla ya matumizi ya computer/laptop per student/teacher haiwezi kumsomesha mwanafunzi mmoja mmoja wa sekondari na chenji zao zikabaki kwenda kuwachangia wale wachache wa elimu ya juu?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…