Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Naam, hili wala halina ubishi. Katika watu ambao hawawezi kukwepa lawama katika kuvuruga chama cha Mapinduzi na hatimaye kuiweka nchi katika sintofahamu na kupelekea nchi kukosa muelekeo ni huyu JK.
1. BIFU LAKE BINAFSI NA EL LILIVURUGA CCM.
Kila mtu anakumbuka jinsi EL alivyokatwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mgombea urais ndani ya chama mwaka 2015. EL alikatwa kihuni, yote hii ni kumfanyia mtima nyongo asiwe mgombea urais kupitia chama hicho. Kila mtu anakumbuka jinsi watu walivyomlalamikia kwa JK kuja na majina ya wagombea mfukoni, kiufupi kuna mambo yasiyo sahihi yalifanyika kwenye kupata wagombea. Tatizo ni kwamba, kila uhuni mmoja unapofanyika, unatengeneza precedence ya uhni mwingine kufanyika mbeleni. Yanayotokea CCM hii leo ya kupitisha wagombea urais wa JMT na ZNZB bila wagombea kujaza fomu ya kuomba kugombea, na bila kupata wadhamini kutoka mikoani, na bila kujadiliwa kwenye vikao vya kamati kuu ni kilele cha matunda ya kutoheshimu haki na kanuni za chama kwenye kupata wagombea na JK hawezi kukwepa lawama kuifikisha CCM hapa.
2. JK ANA UHUSIANO NA SIRI GANI NA SSH HADI KUIFIKISHA CCM HAPA?
Aliyewahi kuwa rais wa JMT hayati JPM aliwahi kusema kuwa SSH hakuwa chaguo lake mwaka 2015, bali chaguo lake lilikuwa ni HM. Akanena kuwa huyu SSH lilikuwa ni chaguo la wazee. Bila shaka hapa JK alihusika kumuwekea JPM huyu mama. Je kuna siri gani ya JK na huyu mama?. Huyu mama alikuwa na merit gani mwaka 2015 hadi afanywe kuwa mgombea mwenza?, alikuwa ameifanyia nini CCM na nchi hadi awe mgombea mwenza?. Hii mbeleko ya kisiasa ambayo huyu mama kabebwa nayo, bila kupita katika chujio lolote serious la kisiasa la kumpa nafasi kubwa kulikoni?, ana nini, au usharika gani na JK?.
3. JK KUSHIRIKI KUMTANGAZA MGOMBEA URAISI KABLA HATA HAJACHUKUA FOMU NI AIBU YA KARNE.
Hii ni aibu kubwa sana kwa mtu aliyewahi kuwa rais, mgombea urais mara kadhaa na mwenyekiti wa chama. Unawezaje kukukubali kubariki na kuwa mnadi mkuu wa uhuni uliofanyika hapo DODOMA?. JK hebu akae chini na ajiulize. Hofu ya kukimbiza mchakato wa uteuzi wa wagombea ni nini. Kama HM hapendwi si uwaache wana CCM waweke mtu mwingine kwani shida ni nini?. Kama kuna watu wanataka kumchallenge SSH si uwaache wamchallenge kwani wewe JK una maslahi gani na SSH au HM hadi ushiriki siasa za "Njama", za "nyuma ya pazia", "siasa za gizani". Au kwa sababu SSH ameendeleza kulinda maslahi yake manono na pia akaenda mbele hadi kupitisha sheria ya kumlipa mkewe mahela mengi kama vile mkewe alivyosuggest?. Je analipa fadhila?.
4. CCM KUPOTEZA USHAWISHI KWA UMMA NA KUGEUKA CHAMA CHA POLISI NA USALAMA.
JK anajua, viongozi wa juu wa CCM wanajua kuwa bila polisi na usalama wa Taifa CCM haiwezi kusimama man to man na upinzani nchini ktk chaguzi. Na hii tabia ya kutegemea polisi na usalama ilifumbiwa macho na JK na viongozi wenzie waliotangualia. Kwa kuwa CCM haitegemei ushawishi wa wanachama wala wananchi, bali wanategenea vyombo vya dola viwape kile wanachokitaka kwa wananchi lakini hawawezi kukipata kwa ridhaa zao. Ndiyo maana wanamlinda HM kwa sababu aliingizwa pale ZNZB kibabe. Na hii michezo hii ya kupora haki za wananchi kuchagua imegeuka na kuwa kama aliyezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi. Leo hii wanachama wa CCM hawana thamani kivile mbele ya kundi dogo la wafanya maamuzi ndani ya CCM kwa sababu hilo kundi dogo linajua lina Polisi na Usalama, wataweka mambo sawa!
5. NAMKUMBUSHA JK KUWA MICHEZO YA KISIASA AKILI NYINGI MBELE GIZA.
Mwaka 2015 alimfanyia figisu EL, akaja na wagombea wa mfukoni. Matokeo yake Chuma kikapenya na kuibuka katikati ya hilo zogo. Chuma kikatandika bakora kila mtu humu nchini, na huyo JK mwenyewe kwa mujibu wa kitabu cha Kabendera alikuwa halali usingizi vizuri, maana chuma kilikuwa kinamvutia rada. Sasa hii hali ya kukwepa haki na kuweka mbele maslahi binafsi na kuleta ujanja ujanja kwenye mambo yanayohitaji utaratibu matokeo yake yanaweza kuwa yasiyodhamiriwa. Awe makini anaweza kuwa anataka aendelee kuonekana ni KING MAKER au MAESTRO wa Kisiasa kumbe anakiumiza chama na anaiumiza nchi na kujivunjia heshima.