Haya ndiyo matunda ya UFISADI, nenda pia hospitali utadhani wagonjwa wametupwa kumbe wamelazwa sehemu inayoitwa ya huduma ya AFYA!, huduma za maji pamoja na mito mikubwa mingi ambayo ni hazina kubwa kwa taifa! huduma hizi MAFISADI wao huzipata kwa gharama yoyote ili mradi tu kama zipo hapa chini ya jua.
Kama kweli BUNGE linajiandaa kuwalinda MAFISADI hii ni balaa, maana CCM hapa tena haidumishi amani bali inaandaa wananchi kupigana vita, maana kusema kweli sasa hivi hali si shwari, ukiona mabango ya maandamano kuongea na mtu mmoja mmoja utajua kabisa sasa hivi hakuna amani bali kuna utulivu tu, kila mtu kakaa hapigani lakini moyo unauma!
JK kama kweli anapiga vita ufisadi sina hakika maana viashiria vinaonyesha chama kime-nunuliwa.
Tusubiri