Chaimaharage
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 211
- 78
Ni wazi kabisa wenzio CCM hawaitaki katiba mpya mchakato ambao uliuridhia. Waliamua kukuunga mkono kama mwenyekiti wao lakini mioyoni mwao hawaitaki kabisa kwa sababu wanajua katiba mpya ambayo itakuwa katiba ya watu ikimaanisha ushirikishwaji wao bila ubaguzi na kushirikisha mawazo yao itakuwa ndio kifo cha CCM wakati wao bado wanataka kula.
Kwa hiyo watauvuruga mchakato kwa kadri wawezavyo ilimradi mpaka tunafikia uchaguzi mwingine katiba mpya iwe bado kama tulivyo shuhudia majuzi Bungeni baadhi ya wabunge wa CCM katika michango yao wakisema uchaguzi ujao ukifanyika kwa kutumia katiba ya zamani itakuwa faida kwao. Kwa hiyo watanzania wenzangu muone kilicho nyuma ya pazia kufuatia vurugu hizi na kupuuziwa hukU. Sasa basi ndugu Jakaya umesemwa kwa mengi mabaya kiasi wengine kufikia kusema awamu hii yako inaisha na hawaoni cha maana kilicho fanyika.
Nakushauri kwa hili la katiba litakujengea heshima miaka 50 ijayo pengine hata kuwazidi watangulizi wako iwapo utatengeneza katiba ya watu. Hakika utaeshimika na kupendwa miaka yote na mabaya yote ya utawala wako yatasahaulika. Mchakato huu wewe pekee ndiye wa kuuokoa sababu kama nilivyo sema hapo juu wenzio hawaupendi na walikulaumu sana kuwasikiliza wapinzani.
Kwa kuwa utawala wako ndio unakwisha huna cha kupoteza, jijengee heshima achana nao, wewe wasikilize wananchi wanataka nini.