Elections 2010 JK Kama Nchi Imekushinda Nipe Mimi

Elections 2010 JK Kama Nchi Imekushinda Nipe Mimi

ibange

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
1,543
Reaction score
553
Kwa wale walioliona gazeti la mwanahalisi leo kuna kijana mdogo hajavaa hata viatu amebeba bango limeandikwa kama kilivyo kichwa cha habari. kwa mtu wa kawaida utacheka basi. ila mimi naona aliyeandaa bango na kumpa mtoto anayeishi ktk mazingira magumu alibeba amefikiria sana na anafikisha ujumbe mkubwa zaidi. kwamba kuna watz wengi ikiwa ni pamoja na masikini wenye uwezo wa kuongoza. ukiwa umeshikilia ofisi ya umma uiheshimu kama dhamana la sivyo tuachie sisi tunaweza, hahahaaa. demokrasia tamu sana
 
duuu si mchezo ampe yeye? na Riz 1 apate nini, huseni Mwinyi je Nape, Makamba Jr, aah hii nchi ndani ya ccm hakuna nafasi ya huyo mtoto kupata nafasi ya uraisi!
 
Kwa wale walioliona gazeti la mwanahalisi leo kuna kijana mdogo hajavaa hata viatu amebeba bango limeandikwa kama kilivyo kichwa cha habari. kwa mtu wa kawaida utacheka basi. ila mimi naona aliyeandaa bango na kumpa mtoto anayeishi ktk mazingira magumu alibeba amefikiria sana na anafikisha ujumbe mkubwa zaidi. kwamba kuna watz wengi ikiwa ni pamoja na masikini wenye uwezo wa kuongoza.

tuwekee hiyo picha p'se!.
 
teeeh teeeh teeeh Dogo analitaka taifa ili ? unajua watu wanadhani urais ni kukaa kwenye msafara wa rais na king'ora. Haya maneno alishaawahi kuyasema Jk na yule JKN akamwambia "bado wewe ni mdogo" alipoomba Luwasa JKN akamwambia "wewe ni mchafu" Luwasa akakimbilia kuoga > sasa Jk kashaona alivoaribiwa saikolojia kwa maneno ya "bado wewe ni mdogo" hadi leo anaisi ni mdogo! Sasa ninaogopa kumwambia bado dogo ni mdogo, hapaana Dogo nchi yako hii, Jiunge na chama cha siasa cha umma tufanye mpango wa kukukabadhi taifa lako!
 
Acha utoto wewe Henge, inawezekana, hii nchi ni yetu na wala sio hao wajinga unaowataja. acha uoga
 
Jamani hili si geni hapa: Omela, kwa wale wataokumbuka nyimbo zetu, aliwahi kuomba NCHI IUZWE KILA MWANANCHI AGAWIWE CHAKE! MI naomba tuaminiane kuwa hata dogo huyu yawezekana kajigundulia kauwezo kama ka babu kuweza kuongoza nji.

Mwisho wa yote meseji imefika.
 
Kwa wale walioliona gazeti la mwanahalisi leo kuna kijana mdogo hajavaa hata viatu amebeba bango limeandikwa kama kilivyo kichwa cha habari. kwa mtu wa kawaida utacheka basi. ila mimi naona aliyeandaa bango na kumpa mtoto anayeishi ktk mazingira magumu alibeba amefikiria sana na anafikisha ujumbe mkubwa zaidi. kwamba kuna watz wengi ikiwa ni pamoja na masikini wenye uwezo wa kuongoza. ukiwa umeshikilia ofisi ya umma uiheshimu kama dhamana la sivyo tuachie sisi tunaweza, hahahaaa. demokrasia tamu sana
Hapo penye nyekundu najiuliza kwanini unafikiri hilo bango halijaandaliwa na huyo mtoto?
Watoto wa siku hizi wanauwezo mkubwa wa kuelewa na kuhoji mambo.
 
Kikwete huwa anawazawadia pipi. Huu ni ujumbe kwake kwamba hawadanganyiki tena na pipi. Wanataka nchi yao, yaani ardhi na raslimali zote zilizomo, kwa ajili yao na maendeleo yao. Wwanataka shule, maji, umeme, waalimu, vitabu, kompyuta nk. Wwanataka wafundishwe kwa vitendo sio nadharia kwamba kompyuta ikitaka kuzima utaona rangi ya bluu, kwamba kuna dude linaitwa ilani ya CCM ndilo linatekelezwa etc
 
bango-kikwete-are-you-corrupted.jpg
 
Back
Top Bottom