Mganji
Member
- May 25, 2011
- 74
- 37
Kutokana na rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuruhusu serikali tatu kwa maana ya serikari ya Tanzania bara, Serikali ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanziba. Rasimu hiyo inapendekeza kuwa aliyewahi kuwa raisi wa Tanzania bara( ambaye kiuhalisia hayupo) au wa serikali ya mapinduzi ya zanziba ni ruksa kugombea uraisi wa Muungano kwa sababu eti hawajawahi kuwa maraisi wa muungano. Kama hiyo ndiyo sababu ya msingi iliyotumika basi ni dhahili kabisa rasimu ijayo ya katiba ya Tanzania bara Katika kipengele cha wagombea urais wa Tanzania bara, wale waliowahi kuwa marais wa muungano wataruhusiwa kugombea uraisi wa Tanzania bara kutokana na sababu inayofanana na ile eti hawajawahi kuwa maraisi wa Tanzania bara. Na hapa ndipo akina Mkapa,Mwinyi na Kikwete watakapo jitupa uwanjani kuwania uraisi wa Tanzania bara.