JK kuileta Real Madrid bongo

Mlalahoi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2006
Posts
2,182
Reaction score
885
Kikwete kuileta Real Madrid

03 Oct 2006
By Mwandishi Wetu

Timu maarufu ya Real Madrid ya Hispania inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo (Primera Liga), itatembelea Tanzania Julai mwakani, Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema jana.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jana Ikulu jijini Dar es Salaam, Kikwete alisema kuwa awali timu hiyo ilitakiwa kuja kufungua uwanja mpya wa michezo utakaofunguliwa mapema mwakani, lakini hawatakuja wakati huo kutokana na kubanwa na mashindano ya ligi na ile ya kimataifa.

Kikwete ambaye alirejea nchini mwishoni mwa wiki akitokea Marekani, alisema kuwa alitembelea Makao Makuu ya Real Madrid wakati walipokuwa wakisubiri kuunganisha ndenge na alipokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Sanchez.

Alisema kuwa makusudio yake yalikuwa kuialika Real Madrid kuja nchini katika ufunguzi wa uwanja mpya wa michezo utakaofanyika Februari au Machi mwakani, lakini licha ya kuupokea mwaliko huo kwa furaha hawataweza kuja kwa kuwa wakati huo watakuwa katika mashindano.

Hata hivyo, uongozi wa Real Madrid umesema kuwa unaweza kuileta timu hiyo Julai au Desemba wakati wakiwa mapumzikoni, ambapo wangependa kuja wakati hali ya hewa ikiwa ya baridi, hivyo Julai ndio mwezi unaofaa.

Rais Kikwete alisema ili kuhakikisha Real Madrid wanakanyaga ardhi ya Tanzania, amekubali sharti la timu hiyo la kutafuta wadhamini wa safari hiyo.

``Jambo la pili walilosema ni kuwa tutafute wadhamini wa safari hiyo. Nimekubali kufanya hivyo, `` alisema Rais katika taarifa yake hiyo iliyozungumzia mambo mbalimbali.

* SOURCE: Nipashe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…