JK kuongoza wafanyabiashara kongamano nchini Afrika Kusini

FJM

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
8,081
Reaction score
6,200
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuongoza wafanyabiashara wa Kitanzania kwenye kongamano la kihistoria la wafanyabiashara litakalofanyika Julai 9 , mwaka huu jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Raymond Mbilinyi, alisema kongamano hilo lililoandaliwa na Tanzania na Afrika ya Kusini, linalenga kukuza fursa za biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

Mbilinyi alisema katika kongamano hilo, Tanzania itaendelea kuwatangazia wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo, usindikaji wa mazao ya kilimo, madini, utalii, uzalishaji wa nishati, ujenzi wa miundombinu, elimu na viwanda.

Source: IPPMEDIA

My take: Kwa nini TIC wasiwaalike hao wafanyabiashara wa Afrika Kusini kuja hapa Tanzania badala ya kwenda kuwalamba miguu huko Pretoria, tena wakiwa na Rais wa Nchi. Nilidhani ingekuwa more effective kama hao potential investors waneona mazingira yenyewe yanayoongelewa badala ya Power Point Presentation! It will be interesting kujua list ya msafara wa Rais though!
 
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuongoza wafanyabiashara wa Kitanzania kwenye kongamano la kihistoria la wafanyabiashara litakalofanyika Julai 9 , mwaka huu jijini Pretoria, Afrika Kusini.
una maana gani JULY 9?
 
una maana gani JULY 9?

Source IPPMEDIA - NIPASHE.
It is possible ni 19th July. Soon Directorate of PRESEDENTIAL' communications itatoa press release ya kuondoka!
 
Julai 9 ina maana gani? Ama ni ya kwako na JK wako. Be care!
 
Julai 9 ina maana gani? Ama ni ya kwako na JK wako. Be care!

Jamani nimesema IPPMEDIA wameweka hivyo Tarehe 9 July!
But my instictc tell me inawezekena ni tarehe 19th July.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…