Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
..mkurugenzi wa mawasiliano IKULU..salva,..mkewe alikuwa amejilipua UK..kama mrundi mkimbizi...SIJUI AMESHAFUTA HIYO STATUS NA KUOMBA UPYA URAIA WA TANZANIA...........ni tanzania amabayo kila kitu kinawezekana ...ikiwemo mtu asiyechujwa kama salva anaweza kupata vetted posts........
haoni tabu au aibu kutumia host ya yahoo...
Bado hajazungumza nadhani itakuwa jioni maana hawakutoa muda hawa waswahili... unless kama ataibukia Bungeni maana ile Gulfstream...
Mkuu BAK, hivi katika suala hili la EPA, baada ya uchunguzi wa Ernst & Young kulikuwa na haja ya kuvuta miguu kweli na kuitisha uchunguzi mwingine?
Pesa za EPA ni kisehemu kidogo tu cha mapesa yaliyokombwa BOT... Naona wamefanikiwa kuweka fix kwenye EPA pekee na watu wamesahau mabilioni mengine yaliyokombwa BoT.
Kazi kweli kweli
Mmeanza kuukana uaraia wenu taratibu?
Uswahili si Uafrika wala Utanzania back to School Kite Munganga. Tena wewe jina lako linaonyesha si mswahili ila unataka kujilipua kama mke wake salva!
PM.. hili la huyu mama nalisikia mara nyingi hapa lakini hakuna mtu ambaye anaweka nyeti hasa ni zipi:
a. Inawezekana vipi mtu kama Salva (kumbuka niliandika makala kumhusu yeye) anaweza kufanya kazi Ikulu bila kuwa vetted?
b. Katika utaratibu huo wa kumvet itawezekana vipi kuwa wamuangalie yeye na isiwe mke wake?
c. Ni ushahidi gani uliopo wa huyu mama kujilipua kuwa yeye ni "mkimbizi" wa Burundi?
Tangu suala hili lilipowahi kuibuliwa huko nyuma na memba mwingine wa huko London nimelifuatilia pembeni na vyote ambavyo nimebahatika kuona ni kuwa huyu mama bado ni Mtanzania na ana pasi ya Tanzania. Kama una chembe yoyote nipenyezee..
Uswahili si uraia bwan kaka. Unajua maana ya Swahili na lilipotokea neno hilo?neno hilo ni neno la kairabu "sahel" kiwa na maana "around the coast" nadhani unawajua watu wa "coast" mfano JK ni Mswahili wa Bagamoyo. Mimi siwezi kuwa Mswahili kwani natokea bara mikoa ya katikati ya Tanzania. Ila mimi ni Mtanzania!Huo ndio uraia wangu.
Na nadhani mtu akisema mswahili ana amanisha tabia hasa za hawa jamaa zetu waswahili "watu wa pwani" umwinyi wao na ajizi kwenye mambo muhimu ndio maana ukiwa na miadi na mswahili "mwinyi" lazima ugande maana atajivutavuta wee huku time nayo ikikimbia maana time huwa haimgoji mtu.
Uswahili si Uafrika wala Utanzania back to School Kite Munganga. Tena wewe jina lako linaonyesha si mswahili ila unataka kujilipua kama mke wake salva!
U cant be serious....
Mzee Mwanakijiji,
Huyu mama alikuwa Luton kama mkimbizi labda kama awe ameondoka sasa. Salva mwenyewe alikuwa mwendaji mzuri wa Luton. Naamini anajua vizuri kwamba mkewe kajilipua hapo.
Kwa Tanzania huenda vetting wanayofanya ni juu ya mhusika mwenyewe na wala sio wake/waume zao.
Kuna uwezekano pia huyo mama ni Mtanzania ila alijilipua kama Watanzania wengine wengi kwa faida ya familia zao.
Mimi simhukumu mtu kwa hili. Kila mtu anayeishi nje amekuja kwa malengo yake. Kuna wengine wamepitia njia rahisi kama shule na kazi lakini wengine hawakuwa na nafasi hiyo ya kuajiriwa kwenye kazi ambazo zingewapatia work permit na hivyo kulazimika kutumia ukimbizi.
Siasa zetu mbaya na umaskini unawafanya watu wachukue maamuzi ya ajabu.