JK, kweli wasanii walihitaji studio?

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
8,191
Reaction score
8,490
bado nashindwa kuelewa nani alimshauri mheshimiwa JK kuwa wasanii wanahitaji studio. ona sasa hata wasanii wenyewe studio hawaitumii au hata wengine wengi hawana taarifa nayo. mimi nadhani washauri wake wamempotosha sana kwenye hili aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya kwa sababu hawakuwashirikisha wahusika wenyewe. kuna gazeti nilisoma kuwa studio hiyo imekabidhiwa kwa T.H.T ambayo hii ni taasisi binafsi ambayo nadhani iko pale kibiashara.je mheshimiwa ametumia taratibu gani kuwakabidhi hiyo studio ambayo naamini imegharamiwa na kodi za wananchi, je wameuziwa na pesa kurudishwa serikalini au mheshimiwa alitumia fedha zake kwa hiyo ana uhuru wa kuamua atakalo? je hakukuwa na uwezekano wa kuikabidhi kwa wizara husika au chama cha wanamuziki kwa usimamizi? karibu wadau kuchangia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…