JK, Lipumba na Seif, Meza Moja.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, leo amekaa meza moja na Mwenyekiti wa CUF, Prof. haruna Lipumba na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamadi katika hali inayothibitisha upinzani wa Tanzania ni kupingana tuu kwa hoja kwenye medani za siasa huku ni marafiki kwa kukumbatiana na kutembea kwa kushikana mik,ono kwa cheko na bashasha za hali ya juu.

Tukio hili limetokea leo jijini Dar es Salaam kwenye Arobaini ya Shani Mloo.

Habari hizi ni kwa mujibu wa Blog ya Michuzi.

Kusema ukweli hizo picha zimenifurahisha sana na kunatakiwa kufanyike matukio ya aina hii as much as possible kabla ya October 2010, ili zitakapo anza pilika za kampeni, kutukanana wataona noma.

Kwa kuziangalia hizo picha jinsi Prof Lipumba na Maalim Seif wanavyofurahi mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo.

"Hadithi hadithi...
.
Shariffu:" Yakhe JK, hivi uliposema wapinzani
hawakabidhiwi nchi ulikuwa unasema kweli?"

Kikwete:" Aaah... Hamtaniwi?. Si mlisikia hata sauti yangu
ilikuwa ya utani utani tuu ili kuwafurahisha CCM
Zanzibar maana mwakani siye hatuna mtu, ni
zamu yako, ila tutasimamisha boya ili
wasitushtukie"

Vicheko vya nguvu.....

Lipumba:" Na huku Bara jee?.

Kikwete: " We Haruni usinipunguzie kura zangu bure,
niache nimalizie ngwe yangu ya pili. Fungu la
kampeni tayari nimeshapeleka Dubai, tena
safari hii, hatujashirikisha majitu mingi, ni
Gavana Mwenyewe na mabenki ya waarabu, si
mliona aibu ya Epa?. Haturudii makosa, wewe
Haruni zamu yako iwe 2015, ilikuwa
tumsimamishe Membe, kwa vile
tumeshakubaliana, basi nitakusimamishia
Masha ili upate mteremko.

Vicheko tena vya asante sana.

Huku akimsindikiza amemshika mkono na kumnong'oneza

Lipumba: " lakini kwenye majukwaa ya siasa, nitaendelea
kuzuga kuisakama CCM kuwazuga Jino kwa
jino au nikiona vipi, nampa bure uenyekiti
wangu Prof Safari na kuhamia kabisa"

Kikwete: "Oh.. No ukihamia utaharibu, tutakosa misaada
tena juzi si ulisikia kuhusu mihela ya IMF,
nimeshapanga nao deal, na migao yao,
Tanzania ndio tutapata mgao mkubwa zaidi,
hivyo ni muhimu tukiendelea kukaza uzi
kuwaonyesha wakubwa na siye tuna
demokrasia ya kweli".

Vicheko tena huku wakimsindikiza kwenye gari yake kwa kuonekana kama wapambe kwa jinsi walivyompamba.

..."Na hadithi yangu ikaishia hapa."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…