Usishangae kauli za JMK zisizo na tija, washangae wanamuziki wala pipi, na maisha rahisi rahisi tu . Hawa jamaa they are very tricky. Wanatafuta wa-tz wanataka nini, wanapenda nini, wanahusudu nini n.k. wanawafuata huko huko. Mawazo ya wanamuziki wa tz ni ya kuiga iga, kuwazawaza ngono, mapenzi, kutajirika kirahisi rahisi tu, umaarufu wa kihivihivi n.k. Sikiliza nyimbo zao utajua ninachokisema. JMK anawapa ahadi za hayo hayo wanayoyataka, wanayoyawaza. Wanamuziki wanamapinduzi umewaona wapi tz, ndo maana wengi wao wanashabikia CCM, sio kwa sababu ya uzuri wake, bali kwa sababu CCM itawapa pipi wanazozitaka. Ndo maana haachi kuwaita 'nyumba nyeupe' kila siku. Very tricky.
Labda nizungunze kwa mfano huu: Ingalikuwa wapiga kura ni watoto wa miaka 2, 3 hivi kwenye kampeni kusingelikuwa na haja ya kuwaambia utawajengea barabara au shule au huduma za maji safi. Ungeliwaambia utawaletea midoli, pipi, biskuti n.k. kwao ndicho cha thamani kuliko hivyo nilivyotaja kwanza. Jamii yetu bado haijapevuka kujua nini tunataka according to priorities kwa sababu ya ulimbukeni wa wa-tz wengi. Ulimbukeni huu CCM hawataki kamwe huondoke, kwani ukiondoka CCM itakuwa chama cha upinzani ghafla. Hizi kofia, t-shirts, shati, 5,000, 10,000 ndicho wa-tz wengi wanachokipa kipaumbele.
Kinachotakiwa ni kuendelea kupiga kelele wa-tz waondokane na ulimbukeni. Waione Kesho bora, yenye matumaini, waachane na pipi na biskuti.