JK na njozi zake za kujijengea heshima kupitia SOKA!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Mwaka 2005 JK alituahidi Taifa Stars itaenda Ghana hatukwenda na sasa kaahidi Taifa Stars itaenda Brazili kila mtu anajua hatuendi sasa ahadi hizi ni za nini?

Wakati JK anahaha na kupoteza maboya yake ili tusahau ya Mtwara ambayo hayuko tayari kuyavalia njuga na kuyamaliza (kama hata ana majibu yake!) kaanzisha zogo la mpira wa miguu na tatizo liko wapi?

Historia ya uongozi wake ni zima moto na hana mipango ya muda mrefu ya kuendeleza lolote achilia mbali soka na ndiyo maana makocha wa nje hudhani ndiyo jibu la kiwango duni kumbe matatizo ni mazito zaidi ya hapo.

Sote tunakubaliana jiko la kiwango ni vilabu lakini huko uwekezaji wa serikali ni sifuri kwa ushauri angelianza na yafuatayo ambayo yataleta chachu ya kweli kwenye soka:-

a) Futa kodi zote kwenye shughuli za michezo.

b) Vilabu kugawana 75% ya mapato ya uwanjani na kuwekewa sheria iliyopitishwa na Bunge.

c) kila mwaka serikali itenge fedha kwaajili ya vilabu kwa mgawo ufuatao:-

i) kila kilabu cha daraja la kwanza kupewa ruzuku ya bilioni moja.

ii) Kila kilabu cha daraja la pili kupewa ruzuku ya robo bilioni kila mwaka

iii) Kila kilabu cha daraja la tatu kupewa ruzuku ya milioni hamsini kila mwaka.

d) Vilabu vyote vinavyotaka kupewa ruzuku tajwa vijisajili soko la hisa na kufuata sheria zote husika zikiwemo za kutoa hesabu za mapato na matumizi hadharani, kuendeshwa kwa misingi ya kampuni n.k

e) Kila mwaka serikali ijenge kiwanja cha kisasa (mradi wa miaka 20)na kukimilikisha kwa kilabu cha daraja la kwanza kwa kuanzia badala ya kusubiria (mfani Azamu) kwenda kuzindua viwanja vya wengineo.

f) Kuanzisha
bahati Nasibu ya Taifa ambayo kazi yake ni kukusanya pesa za kutekeleza ushauri huu. Wakati umefika wa kumwambia Abbas Tarimba "his gamemanship" at Bahati Nasibu ya Taifa is over for we need true professionals to run that vital entity.

..............................baada ya miaka kumi ya utekelezaji wa haya na mengineyo mengi tuongelee AFCON and FIFA WORLD CUP.

IT IS TIME TO GET SERIOUS na kuachana na hizi zima moto, please, Mr. President!
 
Sidhani kama ni logical kwa mtu whether Rais au mtu mwingine kusema kuwa Tanzania itacheza kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia. Ingekuwa rahisi hivyo mbona ungekuta tumeshazicheza mara nyingi?

Nakumbuka Ivory Coast, Rais wao aliweka target ya miaka 20 kwa nchi hiyo kuchezea Fainali za Kombe la Dunia.

Walitumia hiyo miaka 20 kuandaa vijana wangali bado watoto, ikiwa ni pamoja na kutengeza sports academies, sera za michezo, institutions, nk.

Kweli baada ya miaka hiyo walifanikiwa kuchezea Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

Hawa akina Drogba, the Toures, na wengine wengi tunaowaona kwenye luninga hawakuibukia from nowhere.

Hao ni product ya long term programmes ambazo nchi yao ilijiwekea.

It takes years, not months, to build a football team.

This is even more difficult when building a national football team because you cannot pick players outside the country.

Pamoja na kufanya vibaya sana kwenye meichezo ya Olympics bado tuna mentality ile ile.
 
Kitu tunachomuoma KIKWETE sio Masuala ya BURUDANI kama SOKA; Tungependa kwa HEKIMA yake Kama Rais wa nchi ajaribu kutatua MATATIZO yanayoikabili NCHI YETU kwa Sasa hivi...

Nadhani akidumisha hilo Mshikamano utakuwepo na yeye ataweza kufurahia Maendeleo ya SOKA NCHINI...

Sasa hivi anamajukumu ambayo anayakimbia; Mfano BOMU la ARUSHA -- Mshitakiwa hadi sasa ni MMOJA mwendesha BAJAJ; Matatizo ya KIUCHUMI ni kwanini Baadhi ya Wananchi ni Mabepari kupindukia wakati wengine wanazidi kuwa Masikini???

AJIRA; Ni kwanini chama tawala kiliamua kuuza VIWANDA vilivyokuwa vinaajiri wananchi; Matatizo ni yalikuwa na UONGOZI MBOVU au FEDHA zinapotkea kifisadi; Ni kwanini Serikali ya Chama Tawala isingeendelea kuvimiliki ili pia iwe sehemu ya kutoa AJIRA kwa Wananchi UNSKILLED na SEMI-SKILLED? Sasa hivi hayo Majengo ya viwanda ni MAGOFU

Wakati tunaendelea kuzaliana na hatuna KAZI??? ELIMU DUNI...

Kwanini asiachane na hiyo SOKA? Ana Issue nyingi za kujibu; Sasa kuna wananchi wanapingana na kauli zake kuhusu GAS huko MTWARA...

Mr. President... UKO WAPI????
 
Aliyoyaombea kura kesha yasahau sasa amebuni miradi mipya kabisa ambayo wapigakura hawana habari nayo!
 
Sidhani kama ni logical kwa mtu whether Rais au mtu mwingine kusema kuwa Tanzania itacheza kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia. Ingekuwa rahisi hivyo mbona ungekuta tumeshazicheza mara nyingi?

Nakumbuka Ivory Coast, Rais wao aliweka target ya miaka 20 kwa nchi hiyo kuchezea Fainali za Kombe la Dunia.

Walitumia hiyo miaka 20 kuandaa vijana wangali bado watoto, ikiwa ni pamoja na kutengeza sports academies, sera za michezo, institutions, nk.

Kweli baada ya miaka hiyo walifanikiwa kuchezea Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

Hawa akina Drogba, the Toures, na wengine wengi tunaowaona kwenye luninga hawakuibukia from nowhere.

Hao ni product ya long term programmes ambazo nchi yao ilijiwekea.

It takes years, not months, to build a football team.

This is even more difficult when building a national football team because you cannot pick players outside the country.

Pamoja na kufanya vibaya sana kwenye meichezo ya Olympics bado tuna mentality ile ile.

soka ikisimamiwa vizuri ni kiwanda kizuri cha kuzalisha ajira lukuki kuanzia kwa vijana na hata wazee kwa maana ya ushauri na usimamizi! Tatizo letu tunatafuta majibu mepesi kwa maswali magumu
 
Wakati JK anahaha na kupoteza maboya yake ili tusahau ya Mtwara ambayo hayuko tayari kuyavalia njuga na kuyamaliza (kama hata ana majibu yake!) kaanzisha zogo la mpira wa miguu na tatizo liko wapi?

Mkuu Rutashubanyuma, Amani ya Bwana iwe nawe.

JK ni mtu wa Ajabu sana, anashindwa Kujua (Inawezekana kwa Makusudi) katika wakati Fulani, Hitaji la Wa Tanzania ni nini.
Jamana, Hivi kweli Leo Tanzania, Hitaji letu Kuu ni Soka???especially Katika Kipindi hiki cha Sakata la Mtwara????
Huyu Jamaa Mbona anatufanya Wa Tanzania Hamnazo Kiasi Hiki!!!!!!
Yaani, anathubutu Kabisa kutoa kauli kama hiyo Hapo JUU???
Mungu Tusaidie Waja Wako
 
Last edited by a moderator:
huwezi ukaendesha nchi bila vipaumbele ukiwa na ndoto za mafanikio. Alivyoingia madarakani akaondoa wizara ya mipango ambayo ndio ilikuwa anaweka vipaumbele na mipango ya nchi akifikiri wizara ya fedha ni kila kitu. Huyu mtu hawezi fanikiwa hata siku moja kwasababu si mtu makini na hana watu makini wa kumsaidia mambo yaende.
 
Nionavyo amekosa mwelekeo kabisa na kwa hiyo hivi sasa ni bora liende tu!
 
huwezi ukaendesha nchi bila vipaumbele ukiwa na ndoto za mafanikio. Alivyoingia madarakani akaondoa wizara ya mipango ambayo ndio ilikuwa anaweka vipaumbele na mipango ya nchi akifikiri wizara ya fedha ni kila kitu. Huyu mtu hawezi fanikiwa hata siku moja kwasababu si mtu makini na hana watu makini wa kumsaidia mambo yaende.

Kama Stars wasingekuwa waliifunga Morocco nyumbani hizi kasheshe wala tusingelikuwa tunaziongelea kabisa. nasubiri kibanio kule Morocco a Ivory Coast khalafu hutasikia akiongelea tena Stars! Kama kiongozi yuko tu kama hayuko haya huwa ndiyo matunda yake. No vision but inconsequential leadership which we will forget very soon about him..
 
IT IS TIME TO GET SERIOUS na kuachana na hizi zima moto, please, Mr. President!

Mkuu Rutashubanyuma, tusitafute sababu, anayoyasema au kuyafanya JK ni taswira ya jamii anayoiongoza after all we elected him to power, didn't we?

Watanzania ndivyo tulivyo hata aje kiongozi gani, tuna tamaa ya kuona matunda mazuri haraka haraka bila kuwekeza jitihada za kutosha.
 
Last edited by a moderator:
Leo wachezaji wamepewa suti kwaujumla
wamependeza na heshima hata wanaposafiri
kwenda Nje ya Nchi.
 
Achana na Mambo ya Ruzuku kwenye Soka, Hata kwenye maeneo mengine ya kiuchumi, Ruzuku hotelewa kwa ajili ya kustimulate competition na foreign economies kitu ambacho hakipo kwenye soka.

Soka ni moja ya eneo ambalo lina fursa kubwa sana za kibiashara, kinachotakiwa ni kuweka miundo mbinu ya kibiashara full stop, Kwa mfano kila club inayoingia ligi ni lazima iwe inasimamiwa na corporate body, alafu TRA wajifunze kuzitax kampuni hizo full stop, kama soka haiwezi kujiendesha kibiashara ni bora kuachana nayo tujaribu mazingaombwe.
 
Mpira ni pesa, team ujengwa kisaikolojia, hii taifa Stars kila kukicha inakuja na sura mpya zaidi ya tatu na wengine wazee kama Kaseja bado wako tu, na Team haina maandalizi yoyote zaidi ya kujua wanatoka kwenye team flan basi watakuwa wanalala vizuri, wanakula vizuri na afya zao zitakuwa imara kimawazo..Kuna vijana wengi sana wazuri ambao nchi inahitaji kuwasuka ili wawe wazuri kufikia kiwango kinachohijika..Nigeria wamesuka team mpya kabisa na matokeo yake sote tumeona walichokifanya uwanjani. Rais aache hizi siasa za kwenye utaalam
 
soka ni soko kubwa la ajira kulikoni. Nenda Spain soka inapewa ruzuku kibao. Kodi zimesimamishwa muda mreefu wakizirudisha soka kule inakufa.
 
Mpira ni pesa, team ujengwa kisaikolojia, hii taifa Stars kila kukicha inakuja na sura mpya zaidi ya tatu na wengine wazee kama Kaseja bado wako tu, na Team haina maandalizi yoyote zaidi ya kujua wanatoka kwenye team flan basi watakuwa wanalala vizuri, wanakula vizuri na afya zao zitakuwa imara kimawazo..Kuna vijana wengi sana wazuri ambao nchi inahitaji kuwasuka ili wawe wazuri kufikia kiwango kinachohijika..Nigeria wamesuka team mpya kabisa na matokeo yake sote tumeona walichokifanya uwanjani. Rais aache hizi siasa za kwenye utaalam

Jana ujumbe aliupata
 
Leo wachezaji wamepewa suti kwaujumla
wamependeza na heshima hata wanaposafiri
kwenda Nje ya Nchi.

Kama Raisi anahongwa suti iwe wachezaji? On serious note....................timu ni uwqanjani siyo kwenye uvaaji kwani wao siyo sehemu ya ulimbwende.
 
Mkuu Rutashubanyuma, tusitafute sababu, anayoyasema au kuyafanya JK ni taswira ya jamii anayoiongoza after all we elected him to power, didn't we?

Watanzania ndivyo tulivyo hata aje kiongozi gani, tuna tamaa ya kuona matunda mazuri haraka haraka bila kuwekeza jitihada za kutosha.

Did we really elect him? I still believe he stole our vote through NEC & TISS!
 
Nadhani shida JK hajui anataka nini hasa kifanyike Tanzania{Hana kipaumbele}!!!!
Naona anacho fanya ni kujaribu kutafuta majibu rahisi kwa maswali magumu!!!
 
Back
Top Bottom