"Baada ya kupima na kuingia kwenye banda kusubiri majibu nikawa najiuliza ikionekana nina virusi vya ukimwi itakuwaje?"
Nimnukuu: "Baada ya kupima na kuingia kwenye banda kusubiri majibu nikawa najiuliza ikionekana nina virusi vya ukimwi itakuwaje?"
Natumaini rais wetu ni mwadilifu; angekutwa ameambukizwa basi angetueleza watanzania kuwa "Ninao" na kuwa "Nitaendelea kuishi kwa matumaini" maana hizi ni zama za uwazi na ukweli.
Meanwhile; wale wataalamu wa ushauri nasaha na kupima naamini wangemshauri aache kujuana kimwili na mkewe (endapo mke angeonekana hajaathirika) na huenda wangemshauri kama muungwana aachie madaraka by 2010 ili asijeanguka ghafla kwani madawa ya kuongeza nguvu yana mabalaa yake.
Hongera JK kama kweli majibu yalotolewa yalikuwa sahihi!
Icadon,
Una hakika majibu yalotolewa ndiyo yenyewe hakuna siri?
Tatizo majibu ya HIV kwa Bongo huwa yanapindishwa. Sipendi kuamini kuwa majibu ya muungwana yalikuwa ya 'kukaanga'.
Walahi!
We mchokozi sasa Invisible! I think you want to hear something that you are not ready to say. Lakini honestly, kuna minong'ono mingi sana kuhusu JK na ukimwi! But they are all unproven. Lakini the same can be said about other politicians na watu maarufu. Hii ni kutokana na vitando vyao katika jamii. Mi nachoona ni muhimu kwamba mtu asipime publicly 'just because' bali iwe kama kitubio, unadhamiria kutorudia tena vitendo vile unavyojua havifai. Maana kama huna virusi ni kama Mungu anakwambia "Nimekusamehe, nenda na usitende dhambi tena' alafu unarudia kosa hapohapo! Sasa si yote ni bure tu!