JK Nyerere alipozindua soko kuu la Kariakoo

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
jk-kariakoo-1080x675.jpg
Katika maktaba leo tuna picha ya kumbukumbu ya uzinduzi wa soko kuu la Kariakoo la jijini Dar es salaam kulikofanywa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Tarehe 8 Desemba 1975, Baada ya kukamilika kwa ujenzi wake ulionza mwaka 1971 jengo lililojengwa na kampuni ya kizalendo ya Tanzania ya Mwananchi Engineering Contractors Company(MECCCO) chini ya Mhandisi Mzee Beda Amuli.

jk-kariakoo.jpg
Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe ikiwa ni ishara kufungua rasmi jengo la soko kuu la Kariakoo la jijini Dar es salaam mnamo Tarehe 8 Desemba 1975.

kariakoo2.jpg

Hivi ndio mwonekano wa sasa wa hali halisi ya soko kuu la Kariakoo ambapo idadi ya wateja na wafanyabiashara imeongezeka maradufu ukilinganisha na miaka hiyo ya mwishoni mwa miaka ya 1970.
kariakoo-new.jpg

Picha ya soko la Kariakoo jijini Dar es salaam ambalo lilipoanzishwa miaka ya 1970 lilikuwa linaweza kuhudumia wafanyabiashara kuanzia 200 hadi 300 ambapo kwa sasa mamia ya wafanyabiashara wameongezeka sokoni hapo.

Chanzo: Maktaba ya kariakoo.
 
Mkuu habari ya mjini sasa hivi ni yanayoendelea Bungeni: Misamaha ya kodi, ujenzi wa nyumba ya TSh 3bn/- lakini tunaambiwa imejengwa kwa TSh 12bn/-, Mahakama ya kidhalimu ya Kadhi, nk!!
 
Kwa akili zako unataka Jamiiforums tujadili hilo tu? Ukikosa cha kuandika kaa kimya.
 
Wewe hushangai kwa nini watu wengi hawachangii mada yako? Anyway, mada yako ni nzuri, subiri wadau waje wachangie, kama watapenda!!
 
Kuliko kuchangiwa na huu upuuzi wako bora isichangiwe. hata hivo hii nimeweka kama historia na taarifa. Itachangiwa na mjukuu wako hata wewe usipochangia.
 
Kariakoo pale ni vurugu tu...! hakuna mpangilio watu wanatengeneza vibanda....bila hata kufuta taratibu za kihandisi za ujenzi wa soko hilo.....! Ni vurugu tu.
 
Kuliko kuchangiwa na huu upuuzi wako bora isichangiwe. hata hivo hii nimeweka kama historia na taarifa. Itachangiwa na mjukuu wako hata wewe usipochangia.

Kumbe na wewe hutaki mada ichangiwe?
 
NimemuelewA vizuri mleta mada kwa sababu hata mm amenifungua nilikuwa sifaham hata soko la kariakoo lilifunguliwa lini.....ila ww buchanan unajitoa faham kutaka kudissapoint mada lakin jamaa kaeleweka
 
Kuliko kuchangiwa na huu upuuzi wako bora isichangiwe. hata hivo hii nimeweka kama historia na taarifa. Itachangiwa na mjukuu wako hata wewe usipochangia.

mwambie.
Watu wengi wamekuwa wakisahau historia ya taifa lao.
Nakumbuka niliwahi kuandika kuhusu kambi ya wakimbizi wa kizungu iliyokuwa Arusha lakini nilikutana na majanga tu ya baadhi ya watu humu.
 
Tafadhali ipost tena hiyo ya kambi ya wakimbizi. Mimi pamoja na wenzangu kadhaa hapa tuko interested
 
jk-kariakoo-1080x675.jpg
Katika maktaba leo tuna picha ya kumbukumbu ya uzinduzi wa soko kuu la Kariakoo la jijini Dar es salaam kulikofanywa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Tarehe 8 Desemba 1975, Baada ya kukamilika kwa ujenzi wake ulionza mwaka 1971 jengo lililojengwa na kampuni ya kizalendo ya Tanzania ya Mwananchi Engineering Contractors Company(MECCCO) chini ya Mhandisi Mzee Beda Amuli.

jk-kariakoo.jpg
Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe ikiwa ni ishara kufungua rasmi jengo la soko kuu la Kariakoo la jijini Dar es salaam mnamo Tarehe 8 Desemba 1975.

kariakoo2.jpg

Hivi ndio mwonekano wa sasa wa hali halisi ya soko kuu la Kariakoo ambapo idadi ya wateja na wafanyabiashara imeongezeka maradufu ukilinganisha na miaka hiyo ya mwishoni mwa miaka ya 1970.
kariakoo-new.jpg

Picha ya soko la Kariakoo jijini Dar es salaam ambalo lilipoanzishwa miaka ya 1970 lilikuwa linaweza kuhudumia wafanyabiashara kuanzia 200 hadi 300 ambapo kwa sasa mamia ya wafanyabiashara wameongezeka sokoni hapo.

Chanzo: Maktaba ya kariakoo.

Nakumbuka wakati soko linafunguliwa nilikuwa nasoma shule ya Msingi mnazi mmoja nikiwa darasa la kwanza, tulipotoka darasani tukakusanyika na watoto wa mitaa ya kariakoo tukaenda kuangalia uzinduzi, huku nyuma wazazi wakawa wamekuja kutuchukua tulikuwa na mdogo wangu hawakutupata almost one hour ndio tunarudi maeneo ya shuleni, tulipigwa na Baba sitasahau mpaka leo nakumbuka.
Lakini lilikuwa soko zuri kwa wakati ule na safi hata ukiingia shimoni ni kusafi Ila limekuwa dogo sana kutokana na wingi wa watu, serikali ingefanya juu chini kujenga masoko mengine ya kisasa zaidi sehemu tofauti tofauti yatakayo kidhi mahitaji ya watu wengi.
 
Hilo shirika lipo wapi saiv (MECCO) NI SERIKALI YA CHAMA GANI IMEHUJUMU SHIRIKA HILI
 
Siku hizi sijui hatuna watu wenye akili tena za kufikiria kujenga masoko mengi kama hili la kariakoo.
 
Back
Top Bottom