SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,889
Source: Majira, Ijumaa 28 Nov 2008
Na Mwandishi Maalumu, Mahenge
RAIS Jakaya Kikwete amesema kiwango cha rushwa katika sekta ya misitu na maliasili kilikuwa kimevuka mipaka na amewataka viongozi nchini kuongeza juhudi za kupambana na hali hiyo kwa vile hiyo ni sekta yenye uwezo wa kuiingizia Serikali mapato makubwa.
Alisema mazao ya misitu na maliasili yana uwezekano mkubwa zaidi wa kuiingizia mapato Serikali kuliko sekta ya wanyamapori.
Tatizo ni kwamba kiwango cha rushwa katika sekta hii kilikuwa kikubwa mno.
"Tatizo kubwa ni kwamba watu katika sekta hii walikuwa wamekaa miaka mingi katika vituo vile vile vya kazi kwa miaka mingi, wakaota mizizi, na wakaweka mitandao ya rushwa na kuiibia Serikali, alisema.
Rais Kikwete alisema hayo juzi alipokuwa akipokea taarifa ya utendaji wa Serikali katika Wilaya ya Ulanga katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani hapa.
Baada ya kuwa ameulizia na kupewa majibu kuhusu hali ilivyo katika Idara ya Maliasili wilayani humo, Rais alielezea jinsi alivyolazimika kuchukua hatua za kusafisha sekta hiyo baada ya kuingia madarakani.
Tatizo kubwa katika sekta hii ilikuwa ni uvunjaji wa sheria na ukosefu mkubwa wa maadili ... ni hali hii iliyonilazimisha kutoa agizo la Rais kuamuru kuwa wote waliokuwa wamekaa katika kituo kimoja cha kazi kwa miaka mitano au zaidi wahamishwe mara moja, alisema Rais na kuongeza:
Najua zoezi hili lilikuwa la gharama kiasi, lakini ilikuwa lazima kulifanya. Maofisa wengi walikuwa wanavuna misitu wanavyotaka; kama mali yao. Walikuwa wanatoa vibali vya uvunaji wa mkaa. Watu walijisahau kabisa. Tulikuwa tumefikia hatua isiyokuwa na heshima kabisa.
Alisema tatizo ilikuwa ni rushwa kukua mno na kwa viwango cha juu na kwamba maofisa walijenga mitandao ya rushwa na kuinyima Serikali mapato.
Kwangu ulikuwa uamuzi mgumu na wenye gharama. Lakini ilibidi tuanzie mahali pa kurekebisha hali hiyo. Angalau tuwasambaze ili waanze upya, ili angalau 'laini' zao za 'michuzi' zivurugike, alisema.
Wakati huo huo, Rais Kikwete alisema Rais hawezi kuwa mahakama ya kutatua migogoro ya miliki za vitalu vya madini na wala suala hilo haliwezi kutatuliwa kwa walalamikaji kuzungukia maofisa wa Serikali.
Alisema njia bora zaidi ni watu kutafuta jawabu mahakamani, badala ya kushinda wanazunguka katika ofisi za Serikali au kumwendea Rais.
My take;
Hivi dawa ya rushwa ni kuwahamisha watu vituo vya kazi au wizara. It never works, never worked for Mramba et al. Mheshimiwa Rais, rushwa (ufisadi) ni kosa la jinai na mahakama ndio sehemu mahsusi kwa kadhia kama hizi.