JK: Sina mpango kuvunja Baraza

Nimeona hayo mahojiano. Sikuamini kama hao ndio wahariri. Tofauti yao na makanjanja iko wapi?
 
Makamap,
Tatizo ni kwamba wengine wameingia kwa nguvu za vibuyu!! kwahiyo hayao maandiko matakatifu is not applicable
soma hapa!
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8263

Kibuyu hata farao alikitumia enzi za Musa lakini kwa mkono mtakatifu kilishindwa.
Ukitumia KIKUBUYu ukafamikiwa jambo lako si kwamba kibuyu hicho kimekusaidia ila ndivyo ilivyokuwa iwe kumbe umejitia tu kwenye Gadhabu la BWana bure.
 

Niliandika ujumbe huu hapo juu baada ya kusoma mahojiano na Rais kwa ujumla wake. Jana usiku nimepata wasaa wa kutazama mazungumzo naye kwa kina Channel Ten na baadaye TVT. Mambo kadhaa nimeyaona ambayo ni vyema yakafanyiwa kazi.

1. Inaelekea Rais alifanya mahojiano na makundi mawili tofauti ya waandishi. Lakini kinachozua mjadala ni kuwa kwa makundi yote mawili muktadha wa uulizaji maswali na pengine hata staili ya maneno vilikuwa vinafanana fanana. Je, ni kwamba waandishi wetu wote wanafirikiria sawa sawa? Au masuala yanayohitaji majibu yako mahususi kiasi kwamba kila mtu akiweka kwenye chumba chake tofauti anauliza swali lile lile? Au ni kwamba waandishi walipewa maswali kabla ama maeneo ambayo Rais angependa kuulizwa? This is just food for thought.

2. Nadhani ni vyema Rais akapunguza vicheko katikati ya kujibu maswali ambayo watanzania wanategemea majibu mazito. Rais anapozungumzia kwamba tumewauzia wawekezaji wapya Shirika la Reli likiwa limekufa kabisa; ama Net Group ndio wakaharibu zaidi Tanesco, Ama Alliance na baadaye Patnership vikashindwa kuiamsha ATCL na kwamba tumetoka ndege 9 mpaka 1 kutokana na utawala mbovu huo nyuma- Rais anapozungumzia hali hizi huku akiangua kicheko; kwa kweli si nzuri. Inakatisha tamaa zaidi! Inawafanya wananchi waanze kujiuliza, hivi ni nani alipitisha yote haya huko nyuma? Kwa nini Rais wetu anacheka? Je, anafurahia? Najua pengine nia ya Rais ni kuonyesha kuwa mambo ni mazuri wananchi wasiwe na wasiwasi, everything is under control. Lakini si kwa staili hii ya kuangua vicheko. Inaharibu zaidi ya kujenga haiba ya Rais.

3. Majibu ya Rais yametoa ahadi tu kuhusu ATCL na TRC, hayajatoa dira kuonyesha mwelekeo. Walau kwenye TANESCO kidogo amegusia sheria ya kuleta ushindani kwenye uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme. Swali la kujiuliza, ni kwa nini Rais hataki kutazama nyuma na kuchukua hatua? Lazima tutatue tatizo la mazingira ya utiwaji saini wa mikataba ama sivyo mambo ya Netgroup, Richmond nk yatajirudia tena? Ni lazima baadhi wa wahusika wachukuliwe hatua ili iwe fundisho.

4. Kuhusu EPA, Rais amekwepa badala yake amesimulia historia tu- na si mwelekeo na msimamo wa Tanzania katika majadiliano hayo. Pamoja na kuwa ameahidi Mramba atazungumza kwa kina, lakini Rais kama mtu ambaye amekuwa kwenye kada ya diplomasia kwa muda mrefu alipaswa kudokeza terms zetu ni zipi. Na kwa jinsi Rais alivyoirudia rudia tarehe 31 kwamba ni tarehe ya makubaliano inaelekea maamuzi yameshafanyika! Hizo terms za agreement kwa nini haziwekwi open? Napata hisia kwamba tunaburutwa- kwa sababu Rais amerudia rudia sana "wakubwa wakisema" "Hatuna cha kufanya" "Take it or leave it"; na ukishakwenda kwenye majadiliano ukiwa na inferiority complex basi chochote kitakuwa hewala!

5. Nimependa jinsi Rais anavyotumia muda mrefu wa maswali kuzunguka kwenye kufafanua mafanikio ya serikali katika huduma za kijamii na miundo mbinu na mipango iliyopo katika eneo hilo. Mathalani ujenzi wa sekondari kata, ujenzi wa baadhi ya barabara. Mpango wa Afya nnchini utakaohusisha Zahanati, vituo vya Afya nk. Na orodha ya barabara zitakazojengwa hususani kupitia MCC/MCA. Lakini wakati wote nimeendelea kujiuliza- hivi mpaka lini nchi yetu inataendeshwa kwa mfumo wa miradi? Kwa kweli maelezo ya Rais yamedhihirisha hofu yangu kwamba hatuongozwi kwa dira thabiti, tunatekeleza miradi. Katika maelezo ya Rais sijaona dira thabiti ya nini mwelekeo wa msingi wa serikali na malengo kwa mwaka unaofuata na kipindi kilichobaki. Kinachoonekana ni vipande vipande vya shughuli. Na karibu miradi yote iliyokuwa inatajwa ni ile ambayo tumefadhaliwa na washirika wa kimaendeleo. MCA, Japan nk.

6. Mahojiano na Rais yamenidhihirishia kwamba pamoja na kwamba kwa kauli Rais amesisitiza hali ni nzuri na anaridhishwa na mwelekeo nao ni PR Gimmick tu yakuonyesha kwamba things are in control, lakini ukimtazama Rais machoni utajua kabisa kwamba haridhishwi na mambo fulani fulani. Hata ile hamasa ya kusema tutafanya hiki na kile au tumefanya hiki na kile kwa ari, nguvu na kasi mpya imepungua sana. Our president appears to be down! If that is the case, is still call upon him to dissolve the cabinet, and not recycling most of the same Ministers. Mr. President should not let himself be drowned with the likes of Lowassa, Karamagi and Kingunge's!

Mambo ni mengi kwa kweli, ningependa kuyasema lakini wakati ukuta..

JJ
 

Naamini washauri wa Rais watayafanyia kazi haya maelezo na mengine ambayo nimeyatoa toka awali.

Lingine ni la kusahau maswali. Katika mahojiano yale ilikuwa mwandishi mmoja anauliza, Rais anajibu na baadaye ndio anauliza mwingine. Lakini kila aliyepewa wasaa alikuwa akiuliza maswali 2 mpaka 4. Sasa Rais akianza kuyajibu hayo 2 au 4; akifika la pili- tayari anakuwa ameshasahau maswali mengine 2 au 1 yaliyobaki. Hili ni suala ambalo linahitaji kurekebishwa. Haya ni baadhi ya mambo ambayo bila kujua yanapunguza imani za baadhi ya watu. Sababu zinaweza kuwa nyingi, na najua wataalamu wa ikulu wa mawasiliano wanazijua. Lakini la muhimu tu, kama Rais ameamua kutoa maelezo marefu kwa swali moja(kama alivyokuwa akifanya) basi ni muhimu yale mengine akayaweka katika maandishi(hints kidogo) ili akimaliza ayarudia. Niliona katika mahojiano alikuwa na note pad na kalamu, lakini alikuwa akiandika mara chache sana wakati maswali yanaulizwa; na kiasi kikubwa alikuwa haandiki! Sasa ikija wakati wa kujibu maswali yanakuwa yameshasahaulika. Ingetokea kwa muulizaji mmoja ningesema ni bahati mbaya. lakini imetokea mara kadhaa. Na suala hili nimeliona katika mikutano yote miwili niliyoitazama! Leo tuko ndani ya nchi watanzania wenyewe, lakini mambo haya yanaweza kutokea vile vile kwenye press conference za ugenini. Hivyo watu wa mawasiliano ikulu nawaombeni mzingatie hili. Communicators are born, but they are also made. Msitake kumfanya Rais wetu aonekane kuwa ni msahaulifu, ni wajibu wenu kwa kuwa taswira ya mawasiliano ya Rais mwisho wa siku ndicho ambacho mnalipwa kwa kodi za wananchi mkijenge na mnawajibu wa kufanya hivyo kwa Rais yoyote atakayekuwa hapo ikulu.

JJ
 

This boy is naive, he does not know that Rais kucheka is part of the art of speeching. Au yeye akiwa kiongozi atakuwa ananuna tu! Shame on him

PM
 
Yaani unataka acheke then alete historia badala ya kujibu maswali ? Now who is naive here wewe ama yeye ?

JK kuongea na wahariri alitumia mbinu anazo pewa na Salva . Hii ndiyo kazi ambayo Salva imempa kula pale Ikulu .JK aliwatafuta wanao kubaliana naye akaongea nao kwa siri . Mikanda ikawa edited kwenye makali ya hoja ndipo wakatoa hizo mlizo sikiliza . I was there japokuwa sikuwa mwana habari ila msikilizaji .Maswali ni ya kupangwa kabisa na ndiyo maana haya yana jitokeza .
 
Alicheka sana walipokuwa wanamwuliza kuhusu Balali, huku wakitumia maneno "amekimbia nchi", alicheka mno kisha akawa anasema "mniwie radhi". Inaelekea hii habari ilikuwa inamchekesha sana, kuna kituko ndani yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…