JK tazama mwezio huyu


Ukweli ni kuwa ni vigumu kujenga hoja na mtu mwenye upeo wa ki-uchambuzi wa aina yako....

Tanzanianjema
 

Mkuu Gottee,

Heshima mbele sana bro, hakuna cha kuongeza hapo maana nyani amepigwa usoni tena mchana kweupeee, na ubarikiwe tu!

Tunawaambia lakini hawasikii, kwamba sio kazi rahisi kutetea mafisadi, maana hawateteeki wala hawasafishiki, na wale wote wanaowatetea mwisho wao utakuwa kama wa mafisadi yaani aibu ya milele!
 


Ukitaka kumpiga nyani ni lazima usimuangalie usoni, yaani mkuu Gottee unanipa raha sana hapa, leo sina kazi tena, duh JF bwana ukifikiri umemaliza kuhesabu vichwa, unakumbushwa na hawa kina Gottee kuwa bado hujamaliza kuhesabu vyote!

Saafi sana, hoja hujibiwa kwa hoja!
 
And this is LAYMAN's analysis....jitahidi kutafuta ukweli zaidi ya kutegemea hizi onface conclusions...

Hoja zingine bwana, yaani huwezi amini zimetolewa na PHDs, duh kweli Tanzania tuna safari ndefu sana!
 
Ukweli ni kuwa ni vigumu kujenga hoja na mtu mwenye upeo wa ki-uchambuzi wa aina yako....

Bwa! ha! ha! ha! ha! unajua Mkulu Gottee, kwa kweli unanidai kesi ya bia bro maana sijawahi kuona this, mtu anapigwa mawe usoni bila huruma namna hii!

Oooh I Love it, maana this is fun, Where we Dare mwanangu!
 
Wazee kuna tetesi nimesikia kutoka kwa watu tofauti kuwa JK hata alipokuwa Wizara ya mambo ya nchi za nje ilikuwa zake kusita kuchukua au kupitisha maamuzi mazito na yanayoweza kuumiza watu ilikuwa sio rahisi kwake, mara nyingi alikuwa anamsukumia PS wake Mzee Luhanjo.....ni kweli hizi story?

Kama ni kweli inawezekana basi ndio maana ikabidi amchukue Mzee Luhanjo kwenda Ikulu na kama picha ni hiyo ndio maana tunaona msimamo hakuna au maamuzi ya ajabu kwenye masuala mengi kama EPA etc ....Tuabarisheni mnaojua zaidi.
 
Najua kuwa siku zote alipokua akisaifri na rais, ilikuwa lazima rais amngoje airport tena ndani ya ndege, kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa duniani rais kumngoja waziri, only in Tanzania.
 
JK asikitishwa msafara wake kurushiwa mawe chunya

Rais Jakaya Kikwete amesikitishwa na kitendo cha wananchi wa Kijiji cha Kanga wilayani Chunya kuurushia mawe msafara wake na kuwajeruhi baadhi ya watu waliokuwa kwenye
msafara huo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC) jana kufuatia habari kwamba msafara wa Rais Kikwete umeshambuliwa kwa mawe na wananchi wa kijiji hicho.

Rweyemamu alisema kuwa Rais Kikwete amesikitishwa na tukio hilo na kwamba lilitokea baada ya kushindwa kusimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho kwa kuwa muda haukuruhusu kufanya hivyo.
"Rais amesikitishwa kwa kuwa alishindwa kusimama na kuwasalimia wananchi, lakini pamoja na hayo mazingira ya jana asingeweza kusimama,"alisema Rwehemamu.

Alisema tukio hilo lilitokea baada ya saa 1:00 jioni na kwamba baadhi ya vijana waliurushia mawe msafara huo baada ya kuona Rais anawapita bila kusimama na kuwasalimia.

Habari na Salim Said na John Stephen
 
Wakati JK anapigwa mawe na watu waliomchagua, Tazameni mwenzie Obama leo St Louis amabako umati wa watu LAKI MOJA walikuwa wanamsikiliza




Obama rocks........whopeeeeeeeeeeeee
I love you Obama...oopps its me, Michelle
 

Kwa mgombea wa CCM kushindwa Tarime tunapaswa kumpongeza JK kwa kuacha DEMOCRACIA ichukue nafasi yake. Wala hakuna Rais yeyote duniani atakayekupa wewe au mwananchi mwingine yeyote maisha bora. Muhimu ni kuhakikisha Nchi ina AMANI, miundombinu inaboreshwa, huduma za kijamii zinaimarishwa,.....halafu watu kwa jitihada zao wenyewe wanajitafutia maisha bora. Haya kwa asiye kipofu anayaona yanafanyika.
 
Starting with an end in mind...good question Chuma.
Wadau,mbona swali halijibiwi?
I would take a crack at this ila,sina wa kumpendekeza.

Hivi nyie watu wazima na akili zenu mnadhani kura ndio inayomweka kiongozi wa kiafrika madarakani?Ingekuwa hivyo basi Kenya leo ingekuwa inaongozwa na ODM na Zimbabwe ingekuwa inaongozwa na MDC. Mafisadi hawatakubali chama kingine kichukue!Wapo tayari kuua kufanya kila kitu ili jambo hilo lisitokee. CCM hata waweke ndoo ya maji itashinda uchaguzi as long as hakuna fair election kura za polling station na zile zinazosomwa makao makuu ya tume always huwa zinatofautiana. (Tally)
 
Starting with an end in mind...good question Chuma.
Wadau,mbona swali halijibiwi?
I would take a crack at this ila,sina wa kumpendekeza.

Babaa Magofuli, naona amempeleka kwenye mapanki na bado anafanya vizuri?? tatizo mawazi ni kina nani sasa ila naweza kumpatia wa sheria awe Mwakyembe kwa sababu wabunge wa upinzani ndio watakaokuwa wengi basi Waziri wa dhahabu kiwira ampe Slaa hope atamake sure mikataba yote inapitiwa.

ila ni ngumu hakuna Mawaziri kabisa wote chokoraa afadhali atafute wote fresh from school tehetehetehe.....................................
 

Endeleaaa, mkuu, I am so sorry, nadhani umekurupuka na kuandika vitu bila kufikiria. Unaniaccuse kuhusu ushabiki, lakini hujakaa kuniuliza kwa nini ninamsupport Obama. Unafikiri ni kwa sababu Babake katoka nchi jirani au mweusi mwenzangu, or whatever. Hapana. Nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu sana kila alichosema na kuandika. Swali langu: je we umefanya hivyo? umesoma vitabu vyake? Unajua philosophy yake?
1. Je unaelewa nyuma ya neno Change kuna maana gani? Ingekuwa ni neno tu mbona McCain alitumia neno Change pia lakini alishindwa kuwashawishi wapiga kura ikabidi atafute slogan nyingine?
Kama unataka kujua Obama ataleta mabadiliko gani hebu tembelea tovuti yake usome kwa makini papers zilizowekwa ambazo ni ndefu na zinaeleza kwa undani anatarajia kufanya nini. Unafiriki endorsement ya wanasiasa kama Kennedys na General Powell na Warren Buffet ni bure? These are highly intelligent people ambao wamepima na kujua kinachoendelea. If you have problems with Kikwete useme lakini usithubutu kufananisha watu wawili who are heaven and earth apart!
2. Kusema kwamba eti Tanzania ni ndogo (sijui kwa saizi) kuliko Marekani si hoja. Umaarufu wa Obama umevuka mpaka wa nchi yake, hebu nenda kaangalia kama JK atapata hata watu 10 akienda Berlin kuongea! Hata McCain hawezi kupata watu! Anachokifanya Obama na mvuto wake kwa watu ni phenomenon ambayo watu wengi wamekubali. JK
3. Kuhusu kupunguza ugaidi: sijawahi kusikia utumbo ulioutaja hapo juu kwamba eti wamarekani wanampigia kura Obama kwa sababu wanaamini eti itapunguza ugaidi?! Hiyo sijui umetoa wapi. Mpaka sasa katika polls zaidi ya nusu ya wamarekani wanampigia kura Obama kutokana na siasa zake za kiuchumi!

Sidhani kama JK anaelewa hata 1% ya kile anachofanya Obama and his vision.
 
Susuviri: Inakera sana watu wanapomfananisha Obama na JK. Tena ni aibu na ushamba vilevile, maana ni vitu viwili tofauti.

Maybe wanaangalie ile ya kupagawisha watu, hapa nakubaliana nao maana kwa kweli JK alipagawisha watu mno. Tofauti ni kwamba wale ambao wamepagawishwa na Obama wanajua kwa nini anawapagawisha na kwa nini wanampenda. Lakini wale ambao JK aliwapagawisha hawakuwa na sababu; ulikuwa ni uzuzu na ushambenga tu. Ndio maana ulikuwa ukiwauliza hivi kwa nini una-mind JK walikuwa wanabaki wakimumunya midomo, ndio maana hata leo anapoboa wamebaki kusonya!

In any case, JK and Obama are two different animals belonging to different kingdoms, phyla, classes and two distinct species!
 

exagerrated, on this case they are the same and will never be different.
 
Kitila,
Una jingine dhidi ya JK au ni huu URAIS wake tu? Watanzania kwa mamilioni hawakuliona lolote la maana kwa JK walibaki kumumunya midomo!
Lakini Tanzania ipo, na yeye ndiye RAIS wetu.
 
ameomba miaka 5 ya kwanza kuwalipa waliomsaidia jamani yeye alitumia fedha za watu kuingia ikulu including EPA..mnafikiri makene ataweza????????????
JF ni mashahidi mungu mpe baraka zako barakobama
 
Ukweli ni kuwa ni vigumu kujenga hoja na mtu mwenye upeo wa ki-uchambuzi wa aina yako....

Tanzanianjema

Huwezi kujenga hoja na 'a layman' as you concluded! Nami nasema siwezi kuongea na mtu ambaye ni lower than an *****, actually you are just a spoiled moron!
 
Originally Posted by Tanzanianjema
Ukweli ni kuwa ni vigumu kujenga hoja na mtu mwenye upeo wa ki-uchambuzi wa aina yako....

Tanzanianjema
!


Huwezi kujenga hoja na 'a layman' as you concluded! Nami nasema siwezi kuongea na mtu ambaye ni lower than an *****, actually you are just a spoiled moron!
 
mimi sioni tatizo kwa obama nadhani atakapo chaguliwa, umakini unakuwa kwa watendaji wa chini yake atakao wateuwa, tatizo la kikwete alitoa ahadi pasipo kuangalia kwa makini juu ya watendaji wa chini aliowachagua, matokeo yake kachagu watu wakuvuluga malengo yake, na kibaya zaidi akateua maswahiba ambao hata wanapovuluga malengo yake inamuwia vigumu kuwawajibisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…