JK unayajua haya?



Mh! Haya ndo matatizo ya ujuaji mwingi. GT sijui fani yako lakini ktk medicine we ni mweupeeeeeeeeeeee pe peeeeeee. Nakupa sababu kwa nini mwananyamala iko hivyo;

1. Ni hospitali ya kisiasa zaidi, si ya kivitendo na kama tujuavyo kwny siasa linaloongelewa silo linalotendwa.
2. Ni hospitali inayofanya kazi ikiwa imekufa!(a dead horse! can u ride it?)
3. Ni hospitali inayopokea wagonjwa wengi kuliko uwezo wake
4. Ni hospitali inayopokea wagonjwa wa kila aina kiuelewa, lakini wengi ni mbumbumbu wanaojifanya kuelewa sana(hasa hasa mishen town wa kinondoni na m'mala)
5. Its a dumping place... mgonjwa anazungushwa wee kwenye viprivate huko, wakiona anakaribia kufa wanamkimbiza m'mala ili afie huko. Hili ndugu wa mgonjwa wanahusika sana. nina mifano hai, ukitaka nitaweza kukutumia kwny PM, sitaki kuexpose majina ya watu.
6. Ni hospitali inayohudumia machangudoa na vibaka kwa wingi baada ya kuumizwa, kujiumiza(septic abortions etc)
7. Ni hospitali isiyokuwa na vitendea kazi kabisaaa mpk wagonjwa wanaenda kununua syringe medukani!(je hiyo ni kazi ya nesi au daktari kuhakikisha kuna vitu hiyo?)
8....... etc etc

In summary, kila uchafu uko pale!

sasa
Unategemea utendaji kazi utakuweje kwny mazingira hayo? Hujui kuwa mtu ukifanya kazi kwny mazingira kama hayo si rahisi kuwa efficient?

Mwisho: Mtapiga kelele, mtawalaumu wafanyakazi, lakini setting ya hospitali au hata wizara kama haitabadilishwa, we'll continue to see a progressive increase in mortality ktk hospitali hiyo!

Ni mtazamo wangu!
 
Kuna habari kuwa anaweza kufa eidha leo au Jumapili


hahaha...kazi kwisha! Kaja mjuaji zaidi! Anyway....i fail to see JK akijua hili atafanya nini! Hii ishu ni ya Wizara ya Afya. Mbunge wa haya maeneo ni nani? Kwa nini msimpelekee malamiko amswali waziri husiku bungeni? Kwa nini usipeleke malalamiko yako direct wizarani? Hapa JF mtaandika wee na kupeana thanks tu! If you are truly concerned, DO SOMETHING FURTHER ABOUT IT!
 


Kite,

Ni rahisi kusema haya kwa kuwa huna ndugu mwanamke aliyefariki au kupoteza mtoto kwenye hizo hospitali, maarufu kwa jina la "chinja chinja".

Mara kadhaa "wanaboronga" kisha wanakimbiza wahanga (huku wakijua hakuna la kufanya) Muhimbili.

Mfumo tuliowekewa (hatukuridhia) wa kuifanya Muhimbili kuwa hospitali ya rufaa peke yake unawaonea watu wasio na uwezo wa kwenda hospitali binafsi.

Usiombe yakukute, hutakuwa na uwezo tena wa kuamini unachosema. Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.

./Mwana wa Haki

P.S. Unachoandika wewe ni sawa na kusema watu wafe tu, asiwajibike yeyote kwa uzembe! ONA HAYA!
 

100%, You hit the bull!
 

Kwa taarifa yako nimetumia Hospitali ya Mwananyamala zaidi ya miaka 25 toka nikisoma mpaka leo hii na ndivyo ninavyoifahamu, lakini good summary fanya angalizo hapo juu kwa Obhusegwe na hilo ndilo tatizo kubwa ambalo Hospital nyingi Tz zinahusika
 
kwakweli mfumo mzima wa tiba hapa TZ Umedorora, uko doro kabisa, hospitali zote za Umma ni vurugu, ugonjwa ambao unauhakika wa kutibiwa ni Maralia na kutahili watoto labda na kipindupindu, mengine yote wanabahatisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…