Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imetoa ufafanuzi kuhusu hoja ya Mwanachama wa JamiiForums aliyetoa malalamiko yake kuhusu baadhi ya huduma za Watumishi wa hapo.
Kusoma zaidi alichoeleza Mdau bofya hapa ~ Tumepata huduma mbovu JKCI upande wa VIP, baadhi ya Watumishi wanahudumia Watu kwa kujuana
Mwanachama huyo alisema upande wa Idara ya V.I.P ya JKCI hawana mawasiliano mazuri na Wagonjwa, pia wanapoulizwa wanakuwa wakali na kutotoa majibu mazuri jambo ambalo anaona linaweza kusababisha matatizo baina ya pande mbili hizo.
UFAFANUZI WA JKCI
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa JKCI, Anna Nkinda anasema “Hakuna kujuana katika utoaji wa huduma zetu, zinatolewa kwa haki, Watumishi wetu wote wanatimiza majukumu yao inavyotakiwa.
“Huduma ya V.I.P ni nzuri na wastani tunaona Wagonjwa 40 kwa siku wa Idara hiyo, hata Wagonjwa wa kawaida wote wanapewa vipaumbele, hakuna huduma za kujuana.
“Mgonjwa akifika mapema anapata huduma mapema pia, hakuna usumbufu wanaopata kwa kuwa watu wetu wanajielewa, hakuna suala la upendeleo.
“Huduma inatolewa sawa kwa mtu yeyote, ukifika wanakihudumia kama wanakujua siku nyingi, watakupokea vizuri na utapata huduma nzuri.
“Ikitokea mtu amejisikia vibaya na yupo kwenye foleni anamwambia Nesi anapata huduma haraka.”