Hii itasaidia sana kwa vijana kuwa na fikra za kizalendo !
Kwa wale waliopitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanajua fika faida ya jeshi hilo kwa nchi yetu.
Nina mawazo kuwa kuwe na kipengele katika katiba mpya ikisisitiza kuwa ni wajibu kwa kila mtanzania aliyefikisha miaka kumi na minane na kuendelea awe amepata mafunzo haya.
Hii itasaidia sana kwa vijana kuwa na fikra za kizalendo na pia kila mtanzania atakuwa tayari kujihami kwa lolote lile kwani kumkabili adui si lazima uwe na silaha, na hata katika kujiokoa kwahitaji mbinu za medani.
Huenda hii mada imeshaletwa jamvini kama tayari mnisamehe bure!

It is wastage of time kama issue ni kujenga uzalendo,kwani hii tayari imeshaonyesha kushindwa kwa kuwa mafisadi wengi tunaolia nao sasa wamepitia huko JKT!
Ikitokea vita watakwenda wanajeshi kwa kuwa hiyo ndiyo kazi walioajiliwa kuifanya!kwani sasa hivi tauna wanajeshi?na kama hawatoshi hatuwezi kuwaongeza?ninachokikataa mimi ni kulazimisha kila mmoja aende JKT kwa sababu ya kujenga uzalendo,hii sikubaliani nayo kwa kuwa hatutaweza kufikia malengo tunayokusudia!Sasa kama itabidi kwenda mpakani na Malawi tutapeleka nani? Wakati wa Idd Amin JKT iliokoa jahazi. Hawa mafisadi bomu likilipuka tu ndio wa kwanza kulala kifudifudi na kupanua midomo kwani wanazijua hizo mbinu. Ufisadi ni kipindi cha mpito tuu na 2015 wakae chonjo kwani watajuta kuzaliwa bongo.