Niliwahi kusoma habari kutoka gazeti moja:
In addition to standard military training, the programme provided training on human rights, civics, and the history of the union of Tanganyika and Zanzibar, and also aimed to impart students with a sense of unity and patriotism.Tanzanian Finance Minister William Mgimwa told parliament last week that 7.5 billion shillings ($4.7 million) will be allocated in the upcoming budget to reinstate the National Service programme.
Initially, only 5,000 high school graduates will be chosen to participate in the programme.
Kwanza hapo kwenye red bold, hayo masomo vijana wetu wanasoma mashuleni, na kama ingekuwa ni kwa ajili ya vijana kufundishwa hayo, waingize silibasi mashuleni.
Pili, Mgimwa alisema serikali itatenga shilingi bilioni 7.5, hivi Tanzania tuna matatizo mangapi muhimu na sugu ambapo hizo pesa kama zipo zingepelekwa huko kupunguza makali ya matatizo hayo, mfano katika elimu na afya vijijini.
Kwa hesabu ya chap chap, kila kijana mmoja atakayejiunga na kambi kati ya 5,000 itawagharimu walipa kodi shilingi milioni 1.128 kwa muda atakaokuwa kambini, hapo hujaweka gharama za wakufunzi, na vifaa. Iko haja kweli ya kukuza uzalendo kabla ya kukuza elimu na afya?
Tatu, baada ya JKT kuvunjwa majengo na nyenzo zote walijirithisha kwa bure au kwa bei chee, hii ni kusema kuwa ikiwa tunataka kuanzisha upya, itabidi serikali ianze kujenga na kununua vifaa vipya. Lakini zaidi ya yote, kama ambavyo pesa zinazotengwa huwa hazipatikani hata robo yake, hilo hilo litatokea kwenye mpango huu.
Pia, iko haja ya kuanzisha Professional JKT ili atakayejiunga akitoka awe naujuzi fulani katika fani ya kijeshi au kiraia na sio kwenda kambini kupigwa mkwanja tu na push-ups tu.
Ushauri wangu, ikiwa TZ inaona iko haja ya kufanya hivyo, kwanza ichukue kama miaka mitano kujiandaa, sio inaamka kutoka usingizini na kuanza ku
rap kile ilichokiota.