MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Winga Mohamed Bakari aliingia dk66 kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya, dk77 alioneshwa kadi ya njano ya kizembe ambayo inashangaza na kama haitoshi dk90+3 akafanya uzembe kwa kumvuta Shomari Kapombe ambaye hakuwa na mpira wala hatari yoyote, jambo lililopelekea penati na timu yake kufungwa. Ni kama aliitaka kadi nyekundu, na alikuwa akicheza kwa maagizo maalum. JKT Tanzania chukueni hatua dhidi ya mchezaji huyu na bodi ya ligi ichunguze tuhuma hizi za upangaji matokeo.
Inafikirisha sana! Vitendo hivi ni aibu!