Si zani kama ni vizuri sana kuji-limit kwenye hayo maeneo uliyotaja ukazani ndo sehemu pekee pa kutokea kimaisha;
si busara kupeana matumaini kwa mambo ambayo baadae itakuja kuonena si msaada: target yako ni JKT na kwenye hizo Security guard Companies, sawa lkn kwa uelewa wangu huko ni kugumu sana kujinasua kimaisha: kwenye hizi kampuni za Ulinzi Ujira wao aulingani na kazi zinazofanyika, watu wanafanyakazi ili mradi tu muda uende lkn si kwamba maisha unaweza kuya-win kiurahisi we just imagine mshahara wa laki na tano(105,000) kwa mwezi unaweza kufanya nini cha maana!
hivyo hivyo JKT hamna kitu ni kuambulia maumivu na suruba zisizo na kipimo utakaa uko kwa miaka 2 au 3 ukipokea posho elfu arabaini(40,000) kwa mwezi, baada ya hapo unaambiwa umehitimu nenda mitaani katafute kazi, mambo ni yaleyale utaambulia kuwa mgambo wa Jiji n.k kwa mshahala wa laki na ishirini(120,000) kwa mwezi, lbd tu kupitia JKT ubahatike upate chance ya kuingia JWTZ hapo unaweza kunusurika.
What to do:
1. Kwa hiyohiyo elimu uliyonayo unaweza fanya makubwa,kama huna kianzio tafuta vikundi vya Ujasiliamari ujiunge navyo, through that unaweza kujipatia kipato, na ukiona walau mambo si mabaya jiunge na chuo cha VETA, ujitafutie ujuzi fulani ambao utakufanya uonekane ni muhimu katika jamii inayokuzunguka na hatimaye kutoka kimaisha. lkn si hayo ya kwenda kusimama mageitini unalinda binadamu mwenzako kwa kipato duni .