JNIA: Wafanyakazi wa LSG SKY CHEFS Wagoma. Ni Wanaotoa huduma za vyakula na viburudishi kwenye ndege iwapo Safarini

JNIA: Wafanyakazi wa LSG SKY CHEFS Wagoma. Ni Wanaotoa huduma za vyakula na viburudishi kwenye ndege iwapo Safarini

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
WAFANYAKAZI LSG SKY CHEFS WAANDAMANA HADI OFISI ZA TUCTA KUDAI HAKI ZAO

Mashirika ya Ndege zaidi ya ishirini yanayofanya safari zake ndani na nje ya nchi huenda huenda yakakosa huduma za vyakula na viburudishi safarini, baada ya wafanyakazi wa kampuni inayotoa huduma hiyo ya LSG Sky Chefs kulalamikia mahusiano mabovu yalipo kati ya wafanyakazi ambao wengi wao ni wanachama wa chama cha CHODAWU na Uongozi wa Taasisi hiyo kukiuka misingi ya haki za binadamu ikiwemo haki na uhuru wa kujumuika..

Wahudumu hao walifika ofisi za TUCTA makao Makuu na hivyo kutohudhuria kazini kwasiku husika ili kwenda kuwasilisha malalamiko yao na malalamiko uyao yasiopofanyiwa kazi yanaweza kusababisha mgogoro mkubwa wa kikazi unaweza kuathiri utoaji wa huduma hiyo baada ya uongozi wa kampuni hiyo kumsimamisha kazi Mwenyekiti wao wa Tawi la Sky wa Chama cha wafanyakazi wa Nyumbani, Hifadhi, Mahoteli, Huduma za Jamii na Ushauri (CHODAWU), na viongozi wengine wa Tawi kwasababu zilizonje ya kisheria ili kuathiri nguvu na mshikamano uliopo wa awafanyakazi/wanachama.

Wafanyakazi hao ambao ni waajiriwa halali wa kampuni hiyo, wamezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam wakati walipofika Makao Makuu ya Ofisi za Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na Makao Makuu ya Ofisi ya CHODAWU, kushinikiza Kampuni hiyo imrudishe Mwenyekiti wao kazini ndani ya masaa 24.

Anthony Hokororo, Katibu Mstaafu wa Tawi hilo la Sky wa Chama cha CHODAWU, amesema kitendo cha uongozi wa kampuni hiyo kumsimamisha Mwenyekiti wao bila kumsikiliza ni makosa kwa mujibu wa kanuni na sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Ikizingatiwa kosa hilo analotuhumiwa alimiza wajibu wake kama kiongozi wa chama na siyo mtu binafsi na hakuna kosa lolote la kisheria kwa wafanyakazi kutokula chakula kilichaoandaliwa na Uongozi au kushirikia tafrija

Mwenyekiti ametishiwa kuchishwa kazi kutokana na madai ya kuwashinikiza wafanyakazi wa kampuni hiyo kutokula nyama choma siku ya wafanyakazi (MEI MOSI). Na viongozi wengine kuwataka wafanyakazi wasisaini Sera mpya zilitolewa mpaka chama wazipitie kuhakiki maudhui yake. Amesema “sababu kubwa ya kumsimamisha Mwenyekiti wao ni madai ya kwamba mwenyekiti huyo aliwashinikiza wafanyakazi kutokula nyama choma iliyoandaliwa na Kampuni hiyo katika kusherekea siku ya wafanyakazi duniani jambo ambalo sio kweli na halinauhalali wowote.

''Siku ya Mei Mosi Ofisi yetu ilikata kutekelezan utamaduni wa muda mrefu wa Kampuni kutoa usafiri kama ilivyokuwa wa kupeleka wafanyakazi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambapo yalifanyika uwanja wa Taifa kwa Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo ilitubidi wenyewe kutoa nauli zetu na kwenda kisha kurudi majumbani, amesema na kuongeza.

''Sasa tunashangaa uongozi chini ya Afisa rasilimari watu kumpa barua Mwenyekiti wetu ya kumfukuza kazi ndani ya masaa 24 kwa kushinikiza watu kutokula nyama choma iliyoandaliwa siku ya mei mosi jambo ambalo sio la kweli kabisa,''alisema

Amesema wamekuwa wakinyanyasika kwa Muda mrefu baada ya Uongozi huu mpya kuingia madarakani lakini hakuna majawabu wanayoyapata hadi kupelekea kuwafukuza wafanyakazi pindi wanapohoji masuala yoyote yale.

''Kufukuzwa kwa Mwenyekiti wetu kumetuumiza sana, tumekuwa tukinyanyasika sana na menejimenti ya Kampuni yetu wamefikia hatua ya kuvunja sheria za nchi...Mwenyekiti wetu amefukuzwa ndani ya masaa 24 na kumpa barua bila kumsikiliza kisa nyama choma walizoziandaa sikukuu ya Mei Mosi,'' amesema na kuongeza

Amesema kutishiwa kuachishwa kazi wa kwa Mwenyekiti wao ndani ya masaa 24 hakujafatwa taratibu wala sheria za mfanyakazi kwani hakupewa nafasi ya kuongea mbele ya uongozi wa kampuni.

Kwa Upande wake Mmoja wa Wafanyakazi hao Hawa Mbwana amesema yeye ni mfanyakazi wa muda mrefu wa kampuni hiyo ila kwa sasa mambo yamebadilika tofauti na miaka ya zamani ambapo mwajiri hathamini wafanyakazi wake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

''Tunaomba wamrudishe mwenyekiti wetu kwa sababu wamemfukuza kazi bila sababu wala kosa, kisa wafanyakazi kutokula chakula wakati Uamuzi wa kula ni hiari ya mtu, sisi tunahitaji kufanya kazi na maendeleo ya kazi,'' amesema

Amefafanua kuwa kumekuwa na ubadhirifu ndani ya kampuni ambapo mara kadhaa wametakiwa wasaini fomu ambazo wao hawazijui ni za nini na baada ya kuhoji uongozi wa kampuni unakuwa mkali na kusababisha migogoro mbalimbali kwa wafanyakazi.

''Ndani ya masaa 24 Mwenyekiti wetu arudishwe kazini na sisi tutarudi kufanya kazi kama zamani. Tunahudumia zaidi ya mashirika ya ndege 20 lakini kuanzia leo tumesimama hadi tupate suluhisho,'' amesema.

Alipopigiwa simu ili ajibu tuhuma tajwa hapo juu; Afisa Rasilimari Watu wa Kampuni hiyo, Elia Mshana alijibu kuwa yupo kwenye kikao, akimaliza ataweza kuongea ila hadi habari hii inachapishwa bado hakuweza kupokea simu.
 
Hii ni international company, Kwa wafanyakazi kugoma inaweza kuleta shida kwa mashirika ya ndege ambayo yanajali sana maslahi na utu wa watu.
 
Back
Top Bottom