Jo makini,fid q,stamina,roma,baba levo,nay mitego madee,sele na wengine someni hapa,

Free ideas

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
3,497
Reaction score
2,026
kiufupi mi ni shabiki namba moja wa muziki na huwa sibagui wanamuziki,napenda Hip hop na bflava pia,kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia muzik wenu pamoja na wasanii wengine lakini naona kuna kitu binafsi kinanikela na sijui kama wenzangu pia wanakereka ama n mm tu.

kiufupi mnafany amziki mzur na kila mtu anapenda sio siri na kiukwel mnajitahidi sana japo mnazidiana uwezo kimashairi.kero yangu ni hii.
kwa nn katika nyimbo zenu mnapenda sana kutaja mlikotokea,mfano arusha,mwanza,kigoma,moro town,binafsi sion sababu hasa ya kila wimbo kutaja arusha(hasa jo makini),maana naamini hii nidalili ya ubaguz wa mashabiki,mfano kwenye shoo uko musoma afu unasema moro town stand up!!,hii maana yake nn???.robo tatu yawimbo mzima unataja mwanza,sa mshabiki wako wa mtwara unategea apate mzuka wa kuusikiliza wimbo huo mara kwa mara??ama kuja kwenye shoo yako huku ukiwa na kawimbo kamoja hako kanakotamba na umetaja mkoa wako kila baada ya stanza mbili?,

skatai kwamba kuna wakati mtu anajiproud alikotoka na kuonesha uzalendo lakini isiwe kila wimbo bali waweza chagua wimbo mmoja wa misifa basi ukaweka kila kitu humo kisha nyimbo zingine ukagusa jamii na mashabiki wako kila mahala tanzania.

mtu anaimba manzese weee afu anaenda piga shooo,ukerewe mwanza,hiv neno manzese pale litakuwa na kazi??,ama unaimba umasifia mwanza ama arusha unategemea upate shooo kenya,rwanda na burundi acha nje.nakereka sana naposkia karibu kila verse mtu kataja mkoa ama mtaa anaotoka afu kisha anasema gemu gumu hakuna shooo,shoo utapata wapi umeimba moro,mwanza na manzese??,kwa nn msiimbe vitu vinavowagusa watu wote bila kujali mipaka ya mikoa ama nchi.


nawapa mfano,diamond nybo zake nyingi anaimba kwa kugenelize makundi yote na hataji mikoa wala mitaa achilia mbali wimbo wa mbagala ambao ukiuchunguza alimaanisha sehem dun na kila mtu hiyo anajua hata watu wa musoma.sijawahi kusikia akiimba kwamba nimetoka kigoma ama wanangu wa kigoma mambo vipi?,nyimbo zake karibu zote zinaskilizika na watu wote na nchi yoyote kama mtu anaelewa kilichoimbwa.

haya maswala ya raisi wa manzese sijui arusha maskani,tanga kwa bibi na moro town ni kati ya vitu ambavyo vinawafanya muone gemu gumu na kwamba mnabaniwa maana mm kama promota siwezi kukuleta lindi uje kuimba eti we raisi wa manzese ama eti,arusha stand up!,ama watu wangu wa kigoma,ama temeke sijui nn!!,

kwa mtindo huu si ajabu kusikia mtu kastaaf muziki bila kufanya shoo hata moja nje ya nchi maana anatunga na kuimba vitu vya humu humu mikoani na tz.binafsi nawapenda sana hasa tungo zenu lakini jaribuni kubadilika jiulizeni kwa nn akina prof jay,diamond,dimmpo,kiba,ay,na wengine kila siku wanapaa mapipa japo huwa wankuja huku europe ama USA kuimba kwenye migahawa,lakini wanapata japo kifuta jasho na wakirudi huko tz wanakua bei ghali.
huwezi kuimba eti wewe raisi wa gheto sijui mitaaa imefanya nn mara manzese afu ukategemea promo ya kukufanya upate shoo hata kenya,tofauti na hapo badilikeni.Sio kwamba hip hop haiuzi kama alivosema madee hapana ila inauza muhimu mjipange tu.sikatai kwamba mnamshabiki wengi na mnapendwa lakini msipoangalia mtaisha kimuziki na kubaki kushirikishwa kama akina nature maana tmk ilikuwa tmk!!,sasa.

unaweza ukawa msaniii mzuri lakini kama huoni mbali utaishia kuwa wa kitaifa zaidi.
jamani samahani kama nimewakera lakini ni mawazo yangu tu.ninaani mtasoma hapa.

jamani mnaruhusiwa kuchangia chochote iwe kukosoa ama kusapotii,nawasilisha kumbuka ni Free ideas
 
waweza pia washaur chochote hawa wasaniii!!
 
wengine watasema mbona wasanii wa nje wanaimba miji na mitaa yao??,lakini kumbuka hawa tayar washajibebea mashabiki na muzik wao sio kama wetu.hawa wa huku wana majina na tayar washatoka na wengine hawafanyi ili kupata shoo ama pesa bali hobby,lakin kwetu huo naamin wengine muzik ndo kila kitu.
 
Naona wa post na kuji comentia mwenyewe.. Hongera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…