Joachim Marunda Kimaryo, Master Jay "MJ" Master Master tu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
JOACHIM MARUNDA KIMARYO, MASTER JAY "MJ" MASTER MASTER TU!!!

Ukiachana na kumwona magazetini, kwa mara ya kwanza, nilimwona angalau katika picha jongefu kwenye video ya SINTOBADILIKA ya MIKE T.
Yeye, Papa Love, na Majani ni MIONGONI mwa watayarishaji wa Muziki huu wa mwanzo kabisa walioenda majuu kupiga kitabu kuhusu Muziki na kuwa sound engineers badala ya kuishia kuwa beat makers.

Mengi ameyafanya kwenye game hii na katuletea vichwa TOFAUTI vilivyotubariki na kazi zao za KITAMBO zinazoishi mpaka leo.

Master Jay ALIFUNGUA MJ PRODUCTION au MJ RECORDS na kufanya kazi na Profesa Ludigo na Marlon Linje na Meneja Deo.

MJ alikuwa na sehemu mbili za studio yake, huku moja akikomaa nayo Ludigo, ambaye alihusika kuwatengeneza MACHIZI WA HATARI (MAPACHA, FID Q, GEEZ MABOVU NA SQUEEZER) lakini pia ALITENGENEZA ngoma nyingi sana za Gospel na zile za dansi hususani za Msondo Ngoma (japo nyingi alihusika Marlon Linje)

MJ aliamua kustaafu kwa hiyari mwaka 2006 na hakuamua kutuacha na upweke. Akatubless na album ya mwisho iliyoitwa PAMOJA NDANI YA GAME.

Mara nyingi amekaririwa akisema aliacha kutengeneza muziki baada ya ujio wa CRUNK, hapo ndipo alipoamua kutundika daruga lakini hakuamua kufunga ofisi badala yake akaamua kutuletea kijana ambaye angeendana na kasi ya vijana wenzake waliokuwa wakipiga CRUNK, na kwa kumbukumbu nyepesi, producer LUCCI ndiye aliyeongoza kupiga CRUNK kwenye ngoma za CP aliyejiita KING OF BONGO CRUNK, lakini pia black Rhyno alipiga BLACK CHATA hapo kwa LUCCI mpaka kufikia kushiriki tuzo kubwa za Channel O kwa video bora ya wimbo ule.

Kijana aliyeachiwa mikoba ya MJ anaitwa Marco Chali, tutamwongelea siku nyingine.

MJ akaibuka na sura nyingine ndani ya muziki kwa kuwa mmoja wa majaji wa shindano la kuibua vipaji liitwalo BONGO STAR SEARCH, sura ambayo amedumu nayo mpaka leo.

Je, ni combination gani ya MJ uliikubali zaidi na unaikumbuka mpaka leo?
1. MJ NA SUGU
2. MJ NA LADY JAY DEE
3. MJ NA WAGOSI
4. MJ NA WATUKUTU (RAS LION NA JOHN WALKER)
5. MJ NA Q CHIEF
6. MJ NA TID
7. MJ NA CRAZY GK
8. MJ NA SQUEEZER
9. MJ NA WAKALI KWANZA
10. MJ NA WAKILISHA
Combination gani kali imesahaulika kwenye orodha hii?
UNAKUMBUKA Nini kuhusu MJ kwenye muziki?
LUAH
MWANDISHI WA AINA YAKE.
1677408053525.jpeg

1677408064976.jpeg

1677408075238.jpeg

1677408082679.jpeg
 
View attachment 2530491
View attachment 2530492
View attachment 2530493
View attachment 2530494
Jamaa ni mtu ambaye muda wote anachangamka.
Halafu ni mtu open sana.
Ngoja ya tutakukumbuka daima milele from MJ prod by ludigo naielewa mpaka leo.
Halafu ile album ya jay d ya kwanza kuna ile ngoma ya nailazimisha furaha tuliona kama level za akina whitney pale mkono wa master.
Sasa ngoma za akina banza za mtaji wa masikini.
Aisee if I could turn back the hands of time
 
Kuna matumbo yalibeba watu na mengine yalibeba viatu.Mj kwenye tasnia ni kama Messi na mpira kafanya kusudi lake la kuwepo duniani.Mama ànaweza akajipiga kifua na kusema tumbo lilibeba kiumbe Cha aina yake katika kizazi Cha Juma na uledi
 
Back
Top Bottom