Joao Felix: Mchezaji wa 3 ghali zaidi katika historia ya mpira atua rasmi Atletico madrid

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Sasa ni rasmi; yule kinda mwenye kipaji kilichotukuka anayetazamiwa kuwa mmoja wa wachezaji bora kabisa duniani Joao Felix amekamilisha uhamisho wake kutoka klabu ya SL Benfica nchini ureno na Kutua klabu ya Atletico Madrid ya nchini Uhispania.

Dau la uhamisho linatajwa kuwa €130 Million ambalo litamfanya kuwa mchezaji wa tatu ghali zaidi katika historia ya mpira akiwa nyuma ya wachezaji wa PSG Kylian Mbappe aliyegharimu €180 Million na Neymar Jr aliyegharimu €222 Million.

Kinda huyo ana umri wa miaka 19 na aliwika zaidi msimu uliopita alipocheza mechi 26 Akifunga goli 15 na kutoa Assist za magoli 9. Toka ameanza kucheza mpira professional amecheza mechi 87 akifunga goli 34 na kutoa assist za magoli 17.

Mshambuliaji huyo ambaye hucheza kama Winger pia ana uwezo mkubwa wa kudribble na kuwachenga mabeki, spidi kubwa, nguvu ya kupiga shots za mbali,mbunifu, hivyo ukiweka na umri wake basi anaweza kuwa mchezaji bora zaidi misimu ijayo.

Anahamia Atletico ili kumrithi Antoine Griezmann anayehamia Barcelona wiki ijayo kwa dau la €120 Million hivyo kurudisha pesa iliyotumika kumleta huyu kinda ambaye alikua akiwaniwa na Man City,Real Madrid, Manchester United na Juventus pia

Kiufupi La liga inaenda kuwa moto msimu ujao ukitazamia hizi sajili za kufuru zinazofanyika.
 
Bado ni pesa nyingi sana izo kumtolea dogo wa 19yrs
Hiyo sio bei yake bali ni Release clause yaani kiasi unachotoa ili kuuvunja mkataba wa mchezaji unayemtaka. Hii pesa imelipwa maana Benfica walikataa kabisa majadiliano na klabu yeyote ile hivyo walichotaka ni pesa yote ilipwe.... Na hii imetokea hata kwa Neymar alitolewa pesa nyingi kuliko thamani yake.

Ila kama wangejadiliana basi thamani yake halisi isingezidi €60 Million. All in all soko la sasa lipo inflated sana wachezaji wanauzwa kwa bei kubwa kuliko uhalisia.
 
Wenyewe wanamwita new Christino Ronaldo, at 19 tayari kashamzidi thamani cr7. Ref cr7 value yake 100$ Labda atakuja kumzidi huko mbeleni.

Nachokiona hapa Atletico Madrid wabajiandaa kupambana ma Madrid na Barca kunyakuwa la liga. Huyu ni mchezaji wao wa 3 kusajili msimu huu.
 


Kabisa mkuu

Atletico wamepanga washambuliaji wa kutosha kama ujumbe kuwa Ligi haitachukuliwa kizembe msimu ujao
 
Ni new Kaka sio Ronaldo, angalia Hata clip zake YouTube sio mchezaji wa pembeni anatokea katikati.
 
Coutinho aliuzwa kwa £142 nadhani huyo dogo atakuwa namba 4 sio 3
Hapana Coutinho ilikuwa imejumuishwa na variables ndio ikafika hapo ila Principle amount iliolipwa ilikuwa around €120 Million.

Sasa huyu dogo hii ni principal amount tu iliolipwa ila coutinho wameweka na variables zinazotokana na mechi atakazocheza,magoli,assist,kukua kisoka na kithamani ambazo sio lazima lazima zilipwe unless ufikie hivyo vigezo utakavyowekewa.
 
ni wa 5 baada neymar, mbappe, coutinho, ousmane dembele.
Mkuu msihesabu variables kama Bonus n.k sababu hizo zinakuja kulipwa pending na kukua kwa thamani ya mchezaji,mechi atakazocheza,magoli atakayofunga n.k

Hivyo anawekwa wa tatu sababu ya principal amount ambayo inalipwa bila masharti au vigezo vya perfomance ya mchezaji kama vya kina dembele na coutinho.
 
Atletico de madrid wanapaswa kumshukuru na kumuheshimu saana el cholo, Diego Simone kawatoa sehemu moja kawaleta sehemu nyingine leo wanajeuri ya kusajili wachezaji ghali..
Kwakweli mkuu toka achukue usukani imekua timu ya kitofauti sana hata points zao kila msimu ni 76+ tofauti na huko nyuma walipokuwa mid table team
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…