Joash Onyango abwaga manyanga Simba adai kuna ubabaishaji mwingi

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,891
Reaction score
8,448
Beki kisiki wa Simba bwana Joash Onyango ametangaza kuachana na timu hiyo na sasa yuko huru kutafuta marisho mapya, huku akisema Simba kuna ubabaishaji mwingi.

-----

UONGOZI wa Simba umefikia makubaliano mazuri ya kuvunja mkataba na beki wake wa kati, Joash Onyango ambaye raia wa nchini Kenya.

Mkenya huyo hivi karibuni ilielezwa kuuandikia uongozi wa timu hiyo barua ya kuomba kuondoka baada kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Huyo ni mchezaji wa tatu hadi hivi sasa ndani ya Simba kuomba kuvunja mkataba wake mwingine ni Mghana, Augustine Okrah na Mohammed Ouattara huku Ismael Sawadogo akiwa katika hatua za mwisho za kuvunja.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimesema kuwa Onyango na uongozi huo wamefanya mazungumzo ya kuuvunja mkataba wa mwaka mmoja wa beki huyo ambayo yamekamilika kwa asilimia mia moja.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa beki huyo tayari ana ofa nzuri klabu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo hivi karibuni iliwasilisha ofa ya kumuhitaji beki huyo kabla ya msimu kumalizika.

“Mazungumzo ya Onyango na uongozi wa Simba juu ya kuvunja mkataba wake yamekamilika, na hivi sasa yupo huru kwenda kuichezea klabu yoyote atakayohitaji kuichezea.

“Pande zote mbili kwa maana ya uongozi na mchezaji mwenyewe mazungumzo yalikwenda vizuri na kufikia muafaka mzuri wa kuuvunja mkataba huo wa mwaka mmoja,” kilisema chanzo hicho.
 
Tunamtakia maisha mema huko aendako
 
Ni kweli Simba Kuna ubabaishaji mwingi sielewi Ally Salim aliwezaje kupewa nafasi mbele ya Kakolanya matokeo tukatolewa michuano ya Azam na pia kujiondoa kwenye mbio za ubingwa mapema.
Lakini Onyango kiwango chake kimepungua sana na amekuwa akifanya makosa ya kujirudiarudia kwa kutofanya maamuzi sahihi kwa wakati na kufanya makosa mengi yaliyosababisha penati kwenye michuano muhimu.

Inabidi Simba waachane naye kwa amani na wachezaji wengine kama Bocco na Mkude wajitathimini kama wanastahili kuendeleza kuchezea Simba
 
Mpira ni ajira, unapopata greener pastures katika career yako hata kama ni mwalimu utahamia penye maslahi.

Ushabiki maandazi huwa ndio unatutoa akili tu kuandika ujinga.
Kama Ruben Navas tuu miaka 26 huyoo uarabuni kwenye hizo grini paschaa!!hakuna kuremba maisha ndio yanataka hivyo""Uzalendo haumei kwenye umaskini haswa umaskini wa kiuchumi"
 
anayeamua nani acheze ni kocha siyo klabu kama taasisi.
 
Simba imekuwa kubwa kuliko Onyango ila uwezo wake haujapungua.

Onyango kiwango alichukuja nacho ndiyo hicho hicho alichonaccho hadi sasa.
 
Dah! Wakati anasajiliwa huyu mwamba, mashabiki lialia walimpamba kweli kweli. Yaani kama ilivyokuwa tu kwa akina Okwah, Okrah, Mlete Mzungu, nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…