Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Let them be!Keep your friends close but keep your enemies even closer!Hivi ni kanuni kama pai mara kipenyo.Ukiigomea unakwama.
 
07 February 2019
Washington America

Mahojiano kamili na Balozi Masilingi na Mbunge Tundu Lissu


Source: VoA Swahili
 
the more they hate ndo the more we like .# Lissu 4 ever
 
Ni kweli kabisa Lisu alikua mgonjwa ; ila kwa matendo yake ya sasa anaonesha kuwa amerejea Tayari.

Hivyo akatimize wajibu wake wa kibunge ama la, hatua zikichukuliwa dhidi yake hawatakua wanamuonea.
 
Atumwe wazuri wa mambo ya nje na ushirikiano wa mapishi akawaombe mabeberu wasimpokee Lissu. Hahahahaaa
 
Kichaa akimwaga mboga?......
 
Kwanza natoa pole kwa Mh Nimrod mkono ambae nae amekuwa nje ya bunge kwa muda mrefu sasa.
Sababu zinazotajwa ni ugonjwa.
Sasa kwa kuwa Bw. Ndugai anajiita ni mpenda usawa. Namwambia akizuia vya Lissu, asisahau na vya Nimrod mbunge wa Butiama.
Ugonjwa hauombwi, nashangaa jinsi Ndugai anavyojitia umungu.

Muda wa kukanyaga sheria sasa. "Tuko vizuri"
 

Nae anafanya kama ya lisu?
 
Tuache siasa,hata ungekuwa wewe ndio muakiri wa Lissu usingemlipa mshahara kutokana na sababu zifuatazo,1.Ukiwa mgonjwa na mwajiri wako anajua mgonjwa umelazwa hospitali utastahili uipwe mshahara sababu upo hospitalini umelazwa na unaumwa,lakini ghafla anakuona mgonjwa haupo hospitalini na hujatoa sababu ya kutokuwepo hospitalini ,halafu anakuona ukiserebuka mdumange kwenye vijiji vya mbali basi ,mosi atakuona umepona na pili atakushangaa kama umepona na unaweza kwenda kucheza ngoma vijiji vya mbali badala ya kurudi kazini hapo si utakuwa umjiachisha kazi.Tushukuru tanzania sio kama nchi za Ulaya au Marekani,haiwezekani mgonjwa ukaonekana mitaani unafanya yako wakati ruksa yako ilikuwa ya ugonjwa halafuuje udai mshahara,hilo ni kosa la wizi na hapo hapo Lissu angekuwa rupango
 
Sehemu gani ya nchi imechafuka? Imechafukaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha tu zinaonyesha Lissu anatembea kwa magogo. Inatosha tu kukuambia Bado mgonjwa. Utaombaje report ya Dr. Wakati humfanyii matibabu mfanyakazi wako?

Sijui hawa watu tuwafahamu vipi? Wanajidai kwamba Lissu hakufata utaratibu ikiwa na maana kuweko kwake nje kimatibabu hakutambuliki. Suala ni kwamba utapokeaje report ya daktari ambaye mgonjwa wake hakufata utaratibu wa kuweko hospitali yake?

La kushangaza ni kwamba Lissu alishambuliwa wakati akiwa kazini, if anything, kama eneo lile, bunge ama wabunge wana bima, basi alitakiwa alipwe na sio kumsimanga kwa kitu cha msingi kama mshahara!

My take: Huyu jamaa anatapatapa kutaka abakie kwenye ile seat pale, nahisi anaona deputy ndio chaguo la kum replace. Imani yangu ni kuwa atatumika kama toilet paper, halafu atupiliwe mbalini. Coming 2020, huyu jamaa atakuwa ni Mtanzania mnyonge kuliko Watanzania wote!
 
Walishindwa kumuua, wameamua kumnyma haki zake. bunge likishasitisha rasmi mshahara wake iwekwe akaunti yake tumchangie
 
Nawashauri wasijaribu kufanya hili, maana kitakachotokea ni jamii kuingia huruma ambayo itaongeza Lissu kupendwa na jamii hiyo lakini pia Jamii kumchukia Ndugai na Serikali kwa ujumla.

Siku jamii ikisema inchangie Lissu baada ya kusimamishiwa mshahara wake serikali isiye anza kutaka majina waliochanga kwa lengo la kuwafinya ni wao wenyewe watakuwa wamechanga karata vibaya.

Ndugai na serikali suala hili ni la kulifikiria upya, lisitekelezwe kwa gadhabu na kukomoa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmechelewesha sana huo uamuzi Ndugai fanyeni haraka. Kama kuna mzigo kwenye akaunti yake nao uchukueni kabisa kufidia, hawezekani tunalipa kodi halafu mnawapa watu kirahisi tu
Uamuzi huu sio sahihi ndugu yangu, ni kujiongezea chuki dhidi ya jamii na kuongeza Lissu kupendwa na wanyonge!! Ikifikia hapo mtataka kujua nani amemchangia Lissu , lkn itakuwa haina msaada tena na zaidi mtakuwa mme double-loose love na credibility kwa wananchi!

Think, think, think....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hawa wanashindwa kuangalia vitu vyakutusaidia nakuwa makini kama na mawaziri kama mpina anasema wavuvi warudishiwe malizao bila mashariti yoyote sasa wanaotekeleza wanasema engine nilazima zikombolewe lakini generector mataa ndio vitatoka bure sasa amesema wapewe Mali zao bila mashariti engine sio Mali zao?kusema au kutamka bila mashariti kwa hali hiyo bado waziri kauli yake inamaana kweli sasa badala ya kuangalia haya mambo yaonezi wapo bize na wivu walisu nani anafatilia nakutekeleza kauli zamwaziri ajipime ajione mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…