Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Wakifanya hivo ndo vizuri ili dunia ijue kwamba maneno ya Tl ni ya ukweli yamewachoma hadi wamemsitishia mshahara.
 
QUOTE="Sixmonth, post: 30335230, member: 483403"]Yani hawa wanashindwa kuangalia vitu vyakutusaidia nakuwa makini kama na mawaziri kama mpina anasema wavuvi warudishiwe malizao bila mashariti yoyote sasa wanaotekeleza wanasema engine nilazima zikombolewe lakini generector mataa ndio vitatoka bure sasa amesema wapewe Mali zao bila mashariti engine sio Mali zao?kusema au kutamka bila mashariti kwa hali hiyo bado waziri kauli yake inamaana kweli sasa badala ya kuangalia haya mambo yaonezi wapo bize na wivu walisu nani anafatilia nakutekeleza kauli zamwaziri ajipime ajione mwenyewe[/QUOTE]
Wanatekeleza maagizo
 
Ajavunja sheria ila njaa zinamsababisha kwenda kulia lia ughaibuni ila usijadanganye kwamba atampiga chini mwenye chama.



Sent using Jamii Forums mobile app

Mwenzio mgonjwa zaidi ya mwaka sasa, Serikali yake na bunge analotumikia hawajampa hela yake ya matibu ambayo ni stahili yake, atakosaje kuwa na njaa??

Subiri na wewe upate janga la kukulaza kwa miezi 6 tu uone mziki wake kama hutapata njaa. Utu ndiyo ubinadamu wa mtu na sio sura ya mtu.
 
Hivi ushahidi( mkeka) alishautoa wa malipo ya Lisu? Mbona anataka kuanzisha lingine wakati moja halijaisha?
Ndugai tunakumbuka ulisema utatuletea ushahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

1. TL ni Mbunge, ameumizwa akiwa kazini, bunge ndiyo linajukumu la kujua matibabu yake, gharama na maendeleo yake na kwa kila kitu SIO chama chake.

2. Kuimarika au kutoimarika kwa TL ni suala la kidaktari na sio kuangalia kwa macho, ni kweli TL akili yake inaonekana kuwa njema kwa sbb hakupata madhara kichwani, ila mwili wake bado kwani huoni anatembea kwa msaada wa magongo? Aidha, TL hapaswi kupangiwa namna ya kutumia muda wake wa mapumziko wakati akiwa bado kwenye matibabu, ni mtu mzima anajua ni nini anachokifanya hivyo apewe uhuru wake anaostahili bila kuingiliwa na yeyote

3. TL anafanya ziara za kueleza na kulalamikia haki zake zinazoporwa/kutokutendewa haki anayostahili, amenyimwa fedha za matibabu, hakuna taarifa za uchunguzi wa kushambuliwa kwake, Bunge limemtelekeza hata kumjulia hali hosp hawakufanya hivyo, na sasa pole wanayotaka kumpa ni kumnyima mshahara wake na kumpokonya kwa mabavu ubunge wake,

4. TL sio mjinga, anachokifanya hadharani ni kutoa taarifa kwamba kuna mambo hayako sawa, wahusika wajirekebishe na watimize wajibu wake, lakn lazima kuna hatua zitafuata kama ukatili ndidi yake utaendeleza kama anavyotaka kufanya Spika Ndugai

5. Kama wanataka kumhoji dereva au TL mwenyewe utaratibu upo na anaweza kuhojiwa popote hata kama ni hosp, nini kinawashinda hao wapelelezi kuwahoji wanaotaka kuwahoji?

TUWE NA HURUMA, TUTANGULIZE NIA NJEMA, TL YUKO HAI ANAJUA KILICHOMPATA ANA AKILI TIMAMU.
 
Hekima kitu bora sana.

Tuitumie katika kuongoza jamii.
Ndugai anachokifanya leo hii, hasije sikitika akifanyiwa na yeye.
 
Ndugai hasomi magazeti, haangalii Voa na hawasiliani na Serikali au mabalozi wao huko USA Belgium na Germany!
Dunia nzima inajua alipo TL isipokuwa Job Ndugai!
 
Speaker nae anachemka awaandikie barua wadhamini wake wamjulishe TL yuko wapi,Wadhamini watawasiliana na daktari wake kisha daktari atawapa majibu kuhusu maendeleo ya mgonjwa.
 
Tehe Tehe Tehe,chukueni hata na lile Cruiser mliuze kabisa ili roho yenu itulie
 
Wenzetu waliombele kwenye mambo ya sanaa ya uongozi huwa wanatumia akili kupambana na washindani wao kisiasa, Kwa kuwanunua,kuwateua,kuwaweka karibu,kutokuhangaika nao,hawa utumia zaidi nguvu kuliko sanaa ya akili kummaliza mshindani wako.Thus ujikuta wakiharibu zaidi.Action yeyeto juu ya Tl itazidi kuwabomoa zaidi dunia inafatilia kila action kumnyma stahiki zake itaiaminisha dunia kumbe ni kweli.
 
Tafadhali tuoneshe report ya daktari yenye kuthibitisha kuwa amepona la sivyo utakuwa mnafiki tuu mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ina maana Spika hamtambui Balozi wetu wa Marekani aliyeshiriki mahojiano ya Radio na TV za VoA?
Balozi ni muwakilishi wa nchi yetu kule na anatambua wazi alikuwa wapi na Mh TL.Kusema ofisi ya Bunge haitambui alipo ni kudharau ubalozi wetu uliokuwa ana kwa ana na Mh TL
 
Sawa kabisa kusimamisha mshahara wa Lissu. Hata mfanyakazi mwingine wa umma ukiwa mgonjwa kwa zaidi ya miezi mitatu na jopo la madaktari wathibitishe kwamba unaumwa kweli, utastaafishwa kwa ajili ya afya yako na kupewa nusu mshahara kwa miezi sita inayofuata. Kama utaendelea kuumwa baada ya hapo basi utastaafishwa moja kwa moja. Kwa Lissu hakuna daktari aliyeleta taarifa na Lissu mwenyewe yuko anazunguka ulimwenguni akitukana mwajiri wake na kuidhalilisha nchi kwa ujumla. Ni sahihi kabisa kusimamisha mshahara wake. Hela zetu za wanyoge kutoka kwenye kodi zisitumike kumlipa mtu ambaye anakwenda kututukana kwa mabwana zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…