Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Mara ya mwisho Tanzania kuona kiongozi aliyeshukiwa kufanya makosa akambiwa ajiuzulu na akatekeleza, ilikuwa ni mwaka 2008 ambapo Lowassa alijiuzulu kutoka kiti cha uwaziri mkuu. Hivi majuzi kuna Waziri alishukiwa kufanya maamuzi "nonsense" akaambiwa ajiuzulu, ikawa kimya.
Lugola alifokewa hadharani na hayati magufuli kwa kuruhusu mkataba mbovu wa vyombo vya zima moto, hakukjiuzulu hadi alipotumbuliwa. Enzi za Nyerere ilikuwa ni kawaida kwa viongozi kujizulu inapoonekana makosa katika maeneo wanayoongoza: mifano hai ni Mzee mwinyi na Mtei, lakini walikuwepo wengi sana waliokuwa anatanguliza barua za kujiuzulu, halafu rais anawapangia sehemu nyingine ( jambo ambalo ni mojawapo ya makosa ya Nyerere wakati huo).
Ndugai kaonyesha kuwa utamaduni wa kujiuzulu bado upo, sasa huko tuendako tunategema yeyote akifanya makosa ajiuzulu bila kusubili kutumbuliwa!