Job Ndugai: Wabunge mkiikataa bajeti mmejivua Ubunge wenyewe kwa mujibu wa Katiba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1624354854283.png

Spika wa Bunge, Job Ndugai amewaambia Wabunge kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 90(2)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Tanzania ana uwezo wa kuvunja Bunge endapo litakuwa limekataa kupitisha bajeti ya serikali iliyopendekezwa.

Ameyasema hayo leo, Juni 22 ambayo ni siku ya kuhitimisha bunge la Bajeti. Ambapo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni 229 wabunge wanapiga kura za wazi kwenye kupitisha bajeti hiyo.

Kwa mwaka wa fedha 2021/22 Serikali imependekeza bajeti ya Tsh. Trilioni 36.26
 
Sasa huyo Ndugai anakuwa kama haijui kazi ya Bunge?

Bunge kazi yake kubwa ni kuikosoa serikali kwa yale mapendekezo watakayokuwa wameyaleta.

Hivi yeye Ndugai anataka Bunge letu liwe la "rubber stamp" pekee?
 
Kwani Ndugai naye siku hizi anaijua Katiba ya Tanzania? Basi tumeendelea sana
 
Ni jambo la muda tu,,, nchi yetu asaiv lolote linawezekana, muda wowote ule...

Ipo siku sheria wanazozitunga zitawarudia wenyewe..
 
Wabunge wanapaswa kuishauri serikali na sio kuruhusu Kila jambo kupita,

Maslahi ni ya watanzania, jambo la msingi zaidi.
 
Sasa huyo Ndugai anakuwa kama haijui kazi ya Bunge?

Bunge kazi yake kubwa ni kuikosoa serikali kwa yale mapendekezo watakayokuwa wameyaleta.

Hivi yeye Ndugai anataka Bunge letu liwe la "rubber stamp" pekee?
Hivi ni lini ulishaona kama vile anajua kazi yake vizuri.....!!?
 
Kitu gani kimemtisha Ndugai mpaka akatamka hayo maneno, labda kuna dalili mbaya kaoneshwa na wabunge wenzake wa CCM hivyo kaamua kucheza na akili zao.
 
Back
Top Bottom