Joe Biden akutwa UVIKO-19

Joe Biden akutwa UVIKO-19

Escobber pablo

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2024
Posts
302
Reaction score
695
Rais wa Marekani, Joe Biden (81) yuko karantini kwa muda baada ya kupimwa na kugundulika kuwa na ugonjwa wa UVIKO-19, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Marekani, White House.

Ugonjwa huo unakuja wakati ambao Biden anakabiliwa na shinikizo kubwa la kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais dhidi ya mgombea mteule wa Republican, Donald Trump kutokana na umri mkubwa na utendaji usioridhisha.
 
Naambiwa ana demantia......ukiongeza umri mkubwa na uviko 19.

Kumbe Marekani nako ni ving'ang'anizi wa madaraka!?
 
Huyu mzee urais umesha mgomea na akipona kipindupindu kinamsubir
 
Kwani bado tu ni uviko 19?Mi nikajuwa utakuwa ushafika uviko 20,any way kibabu Joe must go.
 
Rais wa Marekani, Joe Biden (81) yuko karantini kwa muda baada ya kupimwa na kugundulika kuwa na ugonjwa wa UVIKO-19, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Marekani, White House.

Ugonjwa huo unakuja wakati ambao Biden anakabiliwa na shinikizo kubwa la kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais dhidi ya mgombea mteule wa Republican, Donald Trump kutokana na umri mkubwa na utendaji usioridhisha.
Sasa si ndio atazidi kujinyea
 
Back
Top Bottom