Jogoo anawika sasa hivi saa Tano Kasoro usiku hapa Shinyanga. Hii ni nini?

Wenge tu hakuna lolote! Pia hiyo hutokea kwa majogoo vijana yan wanaochipukia, huwa wakiwika mchana wanapigwa hvyo husubiri usiku ili wawike kwa uhuru
 
Ukichunguza lazima hapo wanapoishi hao jogoo kwa nje kuna bulb au Mwanga Mara nyingine wanaassume kuwa kumeanza kukucha yaani saa 11 alfajiri

Kama ni mahali penye giza totoro kama kijijini huwezi kusikia jogoo anawika mida hiyo, mpk ifike alfajiri saa 11

Hao ni jogoo wa mjini, taa inawachanganya
 
Jogoo wa dar muda wote wanawika..mwanzo ilinishangaza kidogo. Sijawahi sikia kuku akiwika saa 6 au saa 8 usiku.
Nilichogundua haya makuku ya kisasa ndio vichwa vyao havijui muda upi ni upi
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Sent from my Redmi 8 using JamiiForums mobile app
 
1. Aliwahi kufungiwa kabla ya muda wake; yaani kabla ya saa 12 za jioni aliswagwa ndani ya banda.
2. Kuna taa au mwanga unaomchanganya na mwanga wa mapambazuko.
3. Yupo tu bored kwa upweke au majike wachache sana hapo anapoishi.
4. ...labda kuna mtu aliplay hii
video karibu nae
 
Aisee ata wangu anazingua.nikiwasha taa ya uani(ndipo banda lilipo) fujo hatari ata saa tatu yeye kuwika .naogopa kumkatisha maisha bado kijana.
 
Reactions: Lee
Imebidi nitafute huu uzi make jogoo bandani simuelewi mda huu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…