Jogoo hawiki kabisa!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu fikiria kwamba, umegundua kwamba, mumeo ameishiwa kabisa nguvu za kiume. Bado umri wenu ni ule wa kati, mnahitaji bado kushiriki jambo hilo au pengine mnahitaji hata watoto bado. Je, kama ni wewe ungefanyaje?
 
Swali lako rahisi na jibu lake ni rahisi sana!
 
kama ishu hiyo imetokea kuna mabango kama milioni mtaani wataalam wa kuongeza nguvu za kiume lazima watahusika..
 
Ni kulia taratibu kimoyo moyo maana utafanyaje sasa
 
Kama ulimpenda kwa dhati lazima utavumilia ili mtafute ufumbuzi wa tatizo hilo kwani kama alizaliwa na nguvu za kiume basi lazima solution yake ipo. Ila kama ndio hamkupendana kwa dhati ndio hapo kasheshe kila siku tunaambiwa mke/mume mwema hutoka kwa bwana tuombe na kusubiri na atakuletea wa kufanana nae na ukimpata wa kutoka kwa bwana hata uwe na tatizo la aina gani atakuvumilia tu.
 
Mimi naamini ndoa ni zaidi ya tendo japo sipingi kwamba sio muhimu. Kwa kuwa ni mume wangu nitamsupport na kumsaidia asijisikie vibaya. Nitamuhakikishia kuwa mapenzi yangu kwake ni unconditional hivyo asiwe na wasiwasi. Nitamshauri na kumsindikiza kuwaona wataalamu (madaktari) kama atahitaji. Kwa kifupi mapenzi yangu kwake yataongezeka zaidi na zaidi.
 
hivi kama jogoo haliwiki utakuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa?[wanaume]
kwa wanawake hapo itakuwa usaliti kwa kwenda mbele...............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…